Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Offen Chikola atimkia JKT Tanzania

CHIKOLA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyejiunga na Yanga, Julai 22, 2025, akitokea Tabora United kwa sasa TRA United, alisaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo, ingawa maisha yake ndani ya kikosi hicho yamekuwa magumu kutokana na ushindani wa kuwania nafasi.

ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Yanga, Offen Chikola amekamilisha usajili wa kujiunga na maafande wa JKT Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili, baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja kandarasi yake na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Nyota huyo aliyejiunga na Yanga, Julai 22, 2025, akitokea Tabora United kwa sasa TRA United, alisaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo, ingawa maisha yake ndani ya kikosi hicho yamekuwa magumu kutokana na ushindani wa kuwania nafasi.

Licha ya kusaini mkataba huo wa miaka mitatu, nyota huyo ameitumikia Yanga kwa miezi sita baada ya dirisha dogo la Januari 2026, kujiunga na Singida Black Stars kwa mkopo, japo alikosa pia nafasi ya kucheza mara kwa mara kikosini humo.

CHIKO 01

Baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza akiwa na Yanga na Singida Black Stars, mabosi wa JKT Tanzania wameinasa saini yake kwa mkataba wa miaka miwili, utakaoanza kutumika kikosini humo kwa msimu wa 2026-2027.

Nyota huyo anakumbukwa zaidi msimu wa 2024-2025, akiwa na kikosi cha Tabora United sasa TRA United, ambacho alikifungia mabao saba ya Ligi Kuu Bara, jambo lililoivutia Yanga kumsajili.

Chikola aliyewahi kuichezea pia Geita Gold, mabao hayo saba aliyofunga katika Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2024-2025, ndio yaliyomfanya awe mchezaji wa TRA United aliyefunga mengi zaidi, akionyesha kiwango kizuri kilichoivutia Yanga kumsajili.

CHIKO 02

Chikola anaungana na Said Mkopi, Ismail Mhesa, Constantine Malimi na Fredrick Magata waliotokea wote Mtibwa Sugar ambayo imeshuka daraja kutoka Ligi Kuu Bara hadi Championship. Mwingine ni aliyekuwa kiungo nyota wa Namungo FC, Geofrey Julius.

Nyota wengine waliojiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2026-2027, ni aliyekuwa kiungo wa Tanzania Prisons, Abdallah Masoud ‘Cabaye’ na mshambuliaji Abdallah Idd ‘Pina’ aliyesajiliwa kwa mkopo akitokea Pamba Jiji.