Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyuma ya pazia kutimuliwa kwa Pedro Yanga

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Ureno, alitambulishwa Oktoba 25, 2026 kuchukua nafasi ya Romain Folz ambapo anaondoka akiwa ameshinda Kombe la Mapinduzi 2026 alipoifunga Azam FC, huku akishindwa kutetea Kombe la Muungano 2026 kufuatia kufungwa bao 1-0 na Simba kwenye fainali iliyochezwa Aprili 29, mwaka huu.

KLABU ya Yanga, imetangaza kumfuta kazi kocha mkuu wa kikosi cha kwanza, Pedro Gonçalves ikiwa imepita takribani miezi mitano na siku 19 tangu atambulishwe kikosini hapo, huku nyuma ya uamuzi huo kukiwa na jambo.

Kocha huyo raia wa Ureno, alitambulishwa Oktoba 25, 2026 kuchukua nafasi ya Romain Folz ambapo anaondoka akiwa ameshinda Kombe la Mapinduzi 2026 alipoifunga Azam FC, huku akishindwa kutetea Kombe la Muungano 2026 kufuatia kufungwa bao 1-0 na Simba kwenye fainali iliyochezwa Aprili 29, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa Mei 6, 2026 na klabu hiyo kupitia mtendaji mkuu, Andre Mtine, imesema: “Uongozi wa Young Africans Sports Club, unapenda kuutaarifu umma kuwa umemfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Pedro Gonçalves.

“Uongozi wa klabu unamshukuru Kocha Pedro Goncalves kwa mchango wake alioutoa ndani ya klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.”

Taarifa hiyo imebainisha kwamba, katika kipindi hiki, kikosi cha Yanga kitakuwa chini ya uongozi wa Kocha Abdihamid Moalin pamoja na Kocha Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu.

Kabla ya Pedro kufutwa kazi, kuna dalili zilionyesha mapema kwamba hana muda mrefu wa kufanya kazi ndani ya klabu hiyo kutokana na kile kilichokuwa kinaendelea.

UJIO WA MOALIN

Pedro ambaye alikuwa mkuu wa benchi la ufundi la Yanga mwenye mamlaka ya kupanga program na matumizi ya mifumo ya uchezaji wakati wa mechi za mashindano, ilionekana kuna changamoto ya kiufundi iliyofanya timu hiyo icheze aina tofauti na ile ambayo imezoeleka na kuendana na wachezaji walio ndani ya kikosi hicho.

Hayo yalielezwa na uongozi wa klabu hiyo katika taarifa yake ya Machi 23, 2026, ilipotangaza kumrudisha Moallin kusaidiana na Pedro. “Changamoto hii ya kiufundi imekuwa sababu ya kuifanya timu kupata wakati mgumu kupata matokeo mazuri na kucheza vizuri pia kwenye baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.

“Hivyo, katika kuitatua changamoto hii, uongozi wa Young Africans Sports Club umefikia uamuzi wa kumuongeza kwenye benchi la ufundi, Kocha Abdihamid Moalin kama Kocha Msaidizi wa Kocha Pedro Goncalves,” ilisema taarifa hiyo ya Machi 23, 2026.

Moalin aliwahi kuhudumu Yanga kama Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi katika vipindi tofauti msimu uliopita 2024-2025 chini ya Kocha Sead Ramovic na Miloud Hamdi na kupata mafanikio ya kushinda Kombe la Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho la CRDB na Kombe la Muungano 2025, ujio wake wakati huo ulionyesha si dalili nzuri kwa Pedro.

Tangu Moallin ametua ndani ya kikosi cha Yanga, timu hiyo ilionekana kubadilika kiuchezaji na kupata ushindi wa mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara kwa ushindi mnono ikizifunga Tanzania Prisons (3-0), Pamba Jiji (3-0) na Mbeya City (6-0), kabla ya kutoka 2-2 na Simba, kisha ushindi wa 1-0 mbele ya KMC ambapo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Pedro.

Mbali na mechi hizo za ligi, pia Moalin alikuwepo wakati Yanga ikifuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya TMA Stars ikishinda 1-0. Pia ikipoteza fainali ya Kombe la Muungano mbele ya Simba kwa bao 1-0, kabla ya hapo ilizifunga Muembe Makumbi City (4-0) hatua ya robo fainali na Azam (2-1) nusu fainali.

Siku chache kabla ya Yanga kufanya uamuzi wa kumleta Moalin, Pedro aliiongoza timu hiyo kucheza mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Bara ikiambulia sare dhidi ya Azam (0-0), TRA United (0-0) na Mtibwa Sugar (1-1), hata hivyo, alikuwa hajapoteza mechi yoyote ya ligi hadi anaondoka.

Kocha huyo ameiacha Yanga ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikikusanya pointi 51 zilizotokana na kushinda mechi 15 na sare sita, haijapoteza.

Pedro aliyetambulishwa Yanga Oktoba 25, 2025, ameiongoza timu hiyo kucheza mechi 19 za Ligi Kuu Bara akishinda 14 na sare tano, hajapoteza.

Kwa upande mwingine, aliisimamia Yanga kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakati timu hiyo ikimaliza nafasi ya tatu kundi B ikikusanya pointi nane zilizotokana na kushinda mechi mbili sawa na sare na ilizopoteza.