Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota Azam arejea Tunisia

NYOTA Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyezaliwa Februari 1, 2003, alijiunga na Azam FC, Agosti 16, 2025, akitokea CS Sfaxien ya kwao Tunisia na kusaini mkataba wa miaka miwili uliotarajiwa kumalizika Juni 30, 2027, japo baada ya kuutumikia mmoja ameondoka kikosini humo.

BAADA ya Azam FC kuachana na aliyekuwa winga wa kikosi hicho, Baraket Hmidi, kwa sasa nyota huyo amekamilisha usajili wake wa kujiunga na Klabu ya Stade Tunisien ya kwao Tunisia kwa msimu ujao wa 2026-2027.

Nyota huyo aliyezaliwa Februari 1, 2003, alijiunga na Azam FC, Agosti 16, 2025, akitokea CS Sfaxien ya kwao Tunisia na kusaini mkataba wa miaka miwili uliotarajiwa kumalizika Juni 30, 2027, japo baada ya kuutumikia mmoja ameondoka kikosini humo.

Licha ya matarajio makubwa kwa nyota huyo tangu asajiliwe, lakini alikosa nafasi ya kucheza kutokana na ushindani wa namba na wachezaji wengine wakiwemo, Idd Seleman ‘Nado’, Mzee Hassan Mzee na Abdul Suleiman ‘Sopu’ waliokuwa chaguo la kwanza.

Kukosa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza, uongozi wa Azam FC ulimtoa mchezaji huyo na kumpeleka Diyala SC ya Iraq kwa mkopo dirisha dogo la Januari 2026, baada ya msimu wa 2025-2026 kumalizika ameachwa na kurudi kwao Tunisia.

Kipindi cha miezi sita aliyoitumikia Azam FC, tangu ajiunge nayo Agosti 16, 2025, nyota huyo alichangia bao moja la Ligi Kuu kwa maana ya asisti, kwenye ushindi wa kikosi hicho wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City, Septemba 24, 2025.

Urejeo wa mawinga, Kipre Junior aliyetokea MC Algiers ya Algeria na Gibril Sillah kutoka Al-Ahly SC Benghazi ya Libya, umechangia zaidi kwa Hmidi kuondoka kikosini humo na kwenda kujiunga na Stade Tunisien.