Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam yamtaka mmoja Simba

AZAM Pict


AZAM FC bado haijafunga milango ya usajili kwa msimu ujao, huku taarifa zikieleza klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo ya kutaka kuongeza mchezaji mmoja wa kigeni kutoka Simba SC, hatua inayoweza kuwa usajili wa mwisho kabla ya dirisha kufungwa Agosti 15, 2026.


Uongozi wa Azam tayari umeweka wazi kuwa nguvu kubwa katika usajili wa msimu ujao 2026-2027 imeelekezwa kwenye eneo la kiungo na sehemu za mbele, ikiamini kuwa kuongeza ubora katika maeneo hayo kutaimarisha ushindani wa kikosi chini ya Kocha Florent Ibenge.


Akizungumza na Mwanaspoti, Rais wa Azam, Nassor Idrissa, amesema bado kuna uwezekano wa kuongezwa mchezaji mmoja wa kigeni kabla ya usajili kufungwa, ingawa hakutaja jina wala nafasi anayocheza.

AZA 01

“Tupo katika hatua za mwisho za kufunga milango ya usajili kwa msimu huu. Tupo katika hatua za mwisho za kumalizia usajili. Nafikiri kutakuwa na ongezeko la mchezaji mmoja ambapo kama tutafanikiwa kumpata basi atakuwa huyo ndiye wa mwisho,” amesema.

Kauli hiyo imeongeza nguvu kwenye taarifa za ndani zinazodai kuwa Azam inafanyia kazi mpango wa kumsajili mchezaji wa kigeni Inno Jospin Loemba kutoka Simba.

Loemba, ambaye amekuwa sehemu ya kikosi cha Simba tangu Januari 2026, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao Azam imeonyesha nia ya kuwaongeza katika kikosi chake, huku mazungumzo yakielezwa kuendelea.

AZA 02

Iwapo dili hilo litafanikiwa, Azam itakuwa imekamilisha sehemu ya mpango wake wa kuongeza nguvu katika eneo la kiungo na mbele, ambalo uongozi umelitaja kuwa moja ya maeneo yaliyolengwa katika usajili wa msimu huu.

“Tumegusa zaidi kiungo kwenda mbele. Kama ujuavyo timu, sehemu ya kiungo ni muhimu sana sababu ndiyo kama kiunganishi cha defence (ulinzi) na attacking (ushambuliaji),” amesema bosi huyo.

AZA 03

Kauli hiyo inaonyesha wazi kuwa Azam haitaki kuongeza mchezaji kwa ajili ya kujaza nafasi pekee, bali inatafuta mchezaji anayeweza kuongeza ushindani na kuingia katika mfumo wa Ibenge akiwa na uzoefu wa Ligi Kuu Bara.

Kwa upande mwingine, iwapo Loemba atatua Azam, atafanya idadi ya wachezaji 12 wa kigeni wanaoruhusiwa kikanuni kutimia baada ya Azam kuwatambulisha Gibril Sillah, Kipre Junior, Caleb Ilese, Taiwo Abdulrafiu, Donovan Makoma, John Mano, Henoc Molia, Lupini Dieumerci, Hassan Mubiru na Henri Stanic. Huku ikiendelea kuwa na Yeison Fuentes Mendoza ambaye ni nyota mmoja pekee wa kimataifa aliyekuwepo msimu uliopita.