Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni Asec Mimosas au AS Far Rabat WCL

CAFWCL Pict

Muktasari:

  • FAS Far ni mabingwa wa 2022, wakati Asec ni mara ya kwanza kutinga fainali ikishiriki kwa msimu wa kwanza, ikifanikiwa kuing’oa Masar ya Misri inayotumikiwa na wachezaji wawili wa Kitanzania, Hasnath Ubamba na Violeth Nicholaus watakaovaana na Mazembe kuwania mshindi wa tatu wa michuano ya msimu wa tano.

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake inahitimishwa leo kwa mechi baina ya AS Far Rabat ya Morocco na Ases Mimosas ya Ivory Coast zitakazokutana katika fainali kuwania taji lililotemwa na TP Mazembe ya DR Congo inayowania nafasi ya tatu dhidi ya Masar ya Misri.

FAS Far ni mabingwa wa 2022, wakati Asec ni mara ya kwanza kutinga fainali ikishiriki kwa msimu wa kwanza, ikifanikiwa kuing’oa Masar ya Misri inayotumikiwa na wachezaji wawili wa Kitanzania, Hasnath Ubamba na Violeth Nicholaus watakaovaana na Mazembe kuwania mshindi wa tatu wa michuano ya msimu wa tano.

Mbali na Kombe, timu hizo zinawania pia zawadi ya Sh1 bilioni sambamba na kukata tiketi ya kuwania raundi ya mtoano ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia la Klabu kwa Wanawake.

Hadi zinafika fainali, AS Far ilimaliza kileleni mwa Kundi A ikianza na suluhu dhidi ya FC Masar, kisha kushinda mabao 2-0 dhidi ya USFAS Bamako ya Mali na ushindi kama huo dhidi ya FC 15 de Agosto.

AS Far iliyocheza pia fainali ya msimu uliopita na kupoteza kwa Mazembe, ilitinga nusu fainali na kulipa kisasi kwa miamba hao wa Congo kwa kuing’oa kwa penalti 4-2, huku ASEC Mimosas yenyewe iliongoza Kundi B kwani ilianza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mazembe, sare ya 1-1 mbele ya JKT Queens na kumaliza na ushindi mnono wa 4-0 kwa Gaborone United.

Katika nusu fainali iliitambia FC Masar kwa bao 1-0 na leo itakuwa na kazi ya kuendelea moto mbele ya mabingwa wa zamani ambao wanapigiwa chapuo la kubeba taji la msimu huu kutokana na uzoefu walionao katika michuano hiyo kulinganisha na wapinzani wao ambao ni wageni kabisa.

Miongoni mwa nyota wanaopaswa kuchungwa katika fainali hiyo ni Habibou Ouedraogo (ASEC Mimosas) mwenye mabao matatu, ni kiungo mwenye kasi na chenga nyingi ambazo zimekuwa na faida kwa timu kitu kitakachowapa kazi mabeki wa AS Far.

Kwa upande wa AS Far, Safa Banouk anapenda kuingia ndani ya eneo la hatari na kufanya mashambulizi ya moja kwa moja kwa walinzi wa timu pinzani.

Ni mchezaji anayetumia mguu wa kulia kwa usahihi mzuri kwenye kupiga mashuti na penalti, akifunga mabao mawili muhimu kwa AS far msimu huu.

Nyota mwingine ni Ami Diallo (ASEC Mimosas) ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga. Katika mechi dhidi ya Stella Club alifunga bao la ushindi kwa timu hiyo 1-0 na kuwafanya mabingwa wa WAFU B.

Ana ufanisi wa kutengeneza hatari kupitia kasi yake na kuingia ndani ya eneo la boksi. Katika mechi dhidi ya Gaborone United alifunga mabao mawili.

Najat Badri wa AS Far huyu ndiye mchezaji aliyedumu muda mrefu kwenye kikosi hicho na ni nahodha tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2017.

Ni kiungo mkabaji lakini ana uwezo mkubwa wa kufunga kwa mashuti ya mbali na fundi wa kupitisha pasi za hatari kwenda kwa viungo washambuliaji hivyo kama atadhibitiwa pasi zake zinaweza zisiwe na madhara makubwa.

Kabla ya fainali itapigwa mechi ya mshindi wa tatu ikiwakutanisha Mazembe walioondolewa nusu fainali na As Far dhidi ya chama la Watanzania wawili FC Masar.

Hii ni mara ya kwanza timu hizo mbili zinakutana wakati ambao kila moja ilionyesha ushindani mkubwa mechi iliyopita.


MABINGWA

Mamelodi Sundowns (2021)

AS Far Rabat (2022)

Mamelodi Sundowns (2023)

TP Mazembe (2024)