Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngumi zilivyoacha makovu kwa mabondia

Muktasari:

  • Licha ya kuwa ni mchezo unaolipa pesa nyingi duniani, pia ni mchezo hatari ambao wengi wanaoucheza wamekuwa wakiangukia sehemu mbaya baada ya kustaafu au baada ya pambano fulani.

LAS VEGAS, MAREKANI: Kuna watu wanafariki dunia kwa sababu ya ngumi. Wengine wanapata vilema, baadhi  wanapata majeraha ambayo yanaacha alama katika maisha yao na kuwafanya wasisahau daima juu ya nyakati ngumu walizokutana nazo ulingoni.

Licha ya kuwa ni mchezo unaolipa pesa nyingi duniani, pia ni mchezo hatari ambao wengi wanaoucheza wamekuwa wakiangukia sehemu mbaya baada ya kustaafu au baada ya pambano fulani.

Leo tumekuletea baadhi ya mabondia waliowahi kupata majeraha makubwa yaliyoacha makovu wakati wanapambana katika mapambano mbalimbali.


Billy Collins Jr vs Luis Resto

Mwaka 1983 kulikuwa na pambano kati ya Luis Resto na Billy Collins Jr ambalo hadi leo limebakia kuwa moja kati ya pambano la ovyo kuwahi kutokea kwenye mchezo huu.

Ilikuwa ni baada ya Panama Lewis, ambaye alikuwa ni meneja wa bondia Resto kudanganya kwa kutoa baadhi ya sponji zilizokuwa kwenye gloves za bondia huyo, hivyo kusababisha ngumi zake ziwe na madhara sana.

Kitendo hicho kilisababisha ngumi zimuingie haswa Collins ambaye baada ya pambano kumalizika alipata upofu wa milele na miaka miwili baadae akajiua. Resto na meneja wake wakafungwa jela miaka miwili.


BADOU JACK vs Marcus Browne, 2019

Jack alichanika katikati ya paji lake la uso wakati pambano lake dhidi ya Marcus Browne la mkanda wa  WBC Silver light heavyweight linaendelea.

Alionekana kama amepigwa na shoka kwenye eneo hilo kwani alichanika sehemu kubwa ambayo pia ilionekana kuingia kwa ndani.

Bondia huyu kutoka Sweden alipata majeraha zaidi baada ya kupigwa ngumi nyingine kwenye eneo hilo raundi ya saba na damu zilizidi kumtoka.

Licha ya majeraha hayo Jack aliruhusiwa kuendelea na akamaliza pambano hilo ingawa alipoteza.


TYSON FURY vs

Otto Wallin, 2019

Tyson Fury alichanwa vibaya sehemu ya pembeni ya jicho lake kushukia shavuni Septemba mwaka jana alipopigana na Otto Wallin.

Majeraha hayo yalisababisha ashonwe nyuzi 47, katika picha zilizopigwa ulingoni zilimwonyesha usoni akiwa amepambwa na damu zilizomrukia hadi kifuani.


MASON CARTWRIGHT vs Darren Tetley, 2018

Ilikuwa ni moja kati ya mechi iliyomwachia  Mason Cartwright majeraha makubwa zaidi.

Wawili hawa walipigana kwa raundi nane tu na baada ya hapo Mason alionekana hawezi tena kuendelea kwa sababu uso wake ulichanika vibaya. Timu ya madaktari waliokuwepo  walishauri pambano hilo limalizwe na Tetley akawa ndio bingwa mpya wa mkanda wa WBO European welterweight champion.


HENRY COOPER vs Muhammad Ali, 1966

Cooper hatosahau alichofanyiwa kwenye mapambano mawili aliyocheza na lejendi wa mchezo wa ngumi Marekani, Muhammad Ali.

Pambano la kwanza la mwaka 1963 aliishia raundi ya tano, lakini lile la pili alilopigana mwaka 1966 ndilo hatolisahau kamwe kwenye maisha yake.

Alivunjwa na kuchanwa kwenye pua yake, bega liliteguka na kwenye jicho lake pia alichanika. Pambano hilo lilisimamishwa raundi ya sita na Ali akapewa ushindi.


EVANDER HOLYFIELD vs Mike Tyson,

Mwaka 1996, Evander Holyfield aliushangaza ulimwengu baada ya kumpiga Mike Tyson ambaye kwa wakati huo ndio alionekana kuwa bondia bora duniani.

Baada ya kupigwa raundi ya 11 kwenye pambano hilo, Tyson akaomba mechi ya marudiano mwaka 1997 na mambo yalikuwa magumu pia kiasi cha kumng’ata Evander sikioni na kutoa kipande cha nyama. Hiyo ikasababisha pambano livunjwe.

Holyfield aliwahi kuzungumzia tukio hilo akisema: “Watu wanaponiangalia mara nyingi huwa wanatazama sikio langu, wanadhani niliondolewa sikio lote”

Hata hivyo wawili hawa walimaliza tofauti zao baada ya tukio hilo.


VITALI KLITSCHKO vs

Lennox Lewis, 2003

Huenda likawa pambano lililowahi kumkasirisha sana Klitschko. Wawili hawa walikutana mwaka 2003 na Lewis alifanikiwa kutetea mkanda wake wa WBC baada ya kushinda raundi sita tu ya pambano hilo ambalo lilivunjwa na akapewa ushindi yeye kutokana na majeraha aliyoyapata Klitschko.

Bondia huyo kutoka Ukraine juu ya jicho lake alichanika vibaya na damu zilikuwa zikimtoka kwa wingi kiasi cha kuhitaji msaada.

Mwamuzi akavunja pambano na kumpa Lewis ushindi kwa kile kilichoitwa ‘Technical KO’ ingawa suala hilo lilimuuma sana Klitschko kwani hadi kufikia muda huo yeye ndio alikuwa akiongoza kwa pointi.


Israel Vazquez vs Rafael Marquez, 2010

Mabondia hawa kutoka Mexico wamekutana mara nne kabla ya kustaafu na katika mapambano yote hayo Vazquez ameangukia pua.

Kwenye pambano lanne Vazquez pia alionekana bado hawezi kumshinda Rafael.

Kama ilivyotegemewa kwenye pambano hilo Vazquez  alipoteza na hali yake ilionekana kuwa mbaya kwani alichanwa vibaya karibu na jicho lake la kushoto na kwa kuliangalia ilionakana kama linataka kutoka.