Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utata ngao ya Yanga kuibwa, TFF yatoa tamko

NGAO Piuct


WAKATI wa Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika Agosti 2, 2026 jijini Dar es Salaam, rais wa klabu hiyo, Hersi Said alitangaza taarifa ya kuibwa kwa taji lao la Ngao ya Jamii waliloshinda mwaka 2025.


Taarifa hiyo ilionekana kuwashtua wengi akiwemo yeye mwenyewe kwani baada ya kutolewa, walionekana kujiuliza maswali mengi ya inawezekanaje hilo kutokea na ilikuwaje na kwanini Ngao.


Hersi alisema: “Kuna taarifa moja ninayo hapa ila hii haijanifurahisha sana.”

“Hivi mnaweza kuamini kuna mtu kaiba Ngao ya Jamii ya mwaka 2025? Wakati tukiwa tunasherehekea paredi yetu ya msimu huu (2025-2026), kuna mtu akapata fursa akaiba taji la 2025.”

“Kwa bahati nzuri taji hili limetengenezwa hapa Tanzania na Mtanzania mwenzetu, tumewasiliana na mamlaka husika watatungenezenea na kutupatia. “Lakini kama kuna mtu analo, jamani turudishieni taji letu. Taji linashindaniwa uwanjani, taji haliibiwi.”

Taarifa hiyo ya Hersi imezua maswali mengi ambayo yameendelea kuibua sintofahamu kwa wadau wa soka hapa nchini.

Mwanaspoti katika udadavuaji wake, limeibuka na maswali ambayo yanahitaji majibu ya kina na siyo taarifa ya juu juu kuhusu upotevu wa taji hilo.

NGA 01

1. LILIIBWA WAKATI GANI?

Ni upi hasa muda ambao taji hilo liliibwa? Kwa mujibu wa Hersi, siku ya paredi ndiyo tukio hilo lilifanyika. Ikumbukwe kuwa Yanga ilifanya paredi hilo Jumamosi ya Julai 4, 2026, ambapo kuanzia Karume msafara ulipoanzia hadi kufika makao makuu ya klabu hiyo Jangwani, picha za video zinaonyesha taji hilo lilikuwepo.  Muda ambao wasanii mbalimbali wanatoa burudani Jangwani, mataji yote ambayo Yanga ilikuwa ikiyatembeza likiwemo Ngao ya Jamii 2025, yalikuwepo. Muda gani mwizi alipata upenyo wa kuliiba?

Ukifuatilia kwa kina, picha za video zinaonesha wakati wasanii wakitoa burudani, pale jukwaani kulikuwa na viongozi wa klabu ya Yanga akiwemo Hersi, wachezaji, watu wa benchi la ufundi, walinzi wa klabu hiyo na baadhi ya waliokuwa wakichukua matukio wakiwemo watu wa kitengo cha habari cha Yanga. Hakuna mtu ambaye asiyehusika aliruhusiwa kupanda jukwaani, liliibiwa wapi.


2. MWIZI ALIPATA UPENYO GANI WA KUONDOKA NALO?

Hili ndilo swali gumu zaidi. Kwa kuwa kombe la aina hiyo si dogo ambalo unaweza kuliweka mfukoni kama simu halafu mwingine asigundue, unabaki kujiuliza aliyeliiba alitumia mwanya gani wa kuondoka nalo bila ya kuonekana wakati eneo hilo lina mashabiki wengi tena wakiwa wanaiunga mkono timu moja tu, huyo mwizi alipita wapi, kumbuka kwenye paredi la Simba kibaka alimuibia Elli Mpanzu simu ambayo ni kitu kidogo kuliko ngao, lakini alikamatwa na kuirudisha, vipi kuhusu hili ambalo ni kubwa.


3. LIMEFICHWA WAPI?

Swali lingine la kujiuliza Ngao hiyo baada ya kuibwa ilipelekwa au kufichwa wapi? Kwa kuwa ni kombe linalotambulika na ni kubwa, hivyo si rahisi kulificha au kuliuza bila kutambulika, wengi wanataka kujua kama lengo lilikuwa kulificha pekee, kuliharibu au kuliondoa kabisa mikononi mwa klabu hiyo, lakini unajiuliza ni kwa faida gani?.

NGA 02

4. KWA NINI NGAO YA JAMII?

Ikiwa taarifa hizo ni sahihi, kwa nini mwizi alichagua Ngao ya Jamii badala ya mali nyingine? Je, ilikuwa ni kwa sababu ya thamani yake ya kihistoria, alama yake kwa klabu au kulikuwa na sababu nyingine nyuma ya tukio hilo?

Ukiangalia siku ya paredi, Yanga ilitembeza makombe matano ya Ligi Kuu Bara iliyoshinda mfululizo, pia kulikuwa na mengine kama Kombe la Mapinduzi 2026. Mwizi akalichagua Ngao ya Jamii ambayo ni kubwa ni kwanini?.

NGA 03

5. KUNA TATIZO LA USALAMA YANGA?

Tukio la aina hii linaibua mjadala mpana kuhusu mfumo wa ulinzi wa mali za klabu hiyo. Je, makombe na nyaraka muhimu huhifadhiwa katika mazingira salama? Je, kuna kamera, walinzi wa kutosha na mfumo wa kudhibiti watu wanaoingia na kutoka katika maeneo ya kuhifadhi mali za klabu?

Kama uliwahi kwenda katika jengo la Yanga, utaungana nami kuhusu ulinzi mkubwa ulioko, kama huna jambo la muhimu linakupeleka pale ni ngumu kuingia kirahisi, sasa mwizi alipita wapi na kufanikisha tukio hilo?

Lakini pia eneo muhimu kama lile haliwezi kukosa kamera ambazo zinaonyesha kila kinachoendelea pale, kama walivyoonyesha tukio la kuibiwa kwa baadhi ya vifaa vya kidigitali miezi kadhaa iliyopita, bila shaka hata tukio hili linaweza kuangaliwa kupitia kamera zilizopo na kumfahamu aliyetenda tukio hilo.


6. WALIRIPOTI SEHEMU HUSIKA?

Katika matukio ya aina hii hatua ya kwanza huwa ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika. Je, viongozi wa Yanga waliripoti katika kituo gani cha polisi? Uchunguzi ulianza lini, na je, mamlaka zilitoa tamko lolote kuhusu mwenendo wa uchunguzi huo?

Kwani taarifa ilitolewa katika mkutano mkuu wa Agosti 2, 2026, zikiwa zimepita takribani siku 29 tangu kufanyike kwa paredi.

Kwa mujibu wa Hersi, taarifa wameipeleka TFF kwa ajili ya kuona uwezekano wa kutengenezewa lingine, hii inaonesha hawakuripoti kituo cha polisi. Kwanini?

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, alisema: “Kombe liliibwa kwenye paredi la ubingwa, lakini nisizungumze sana kwa sababu tunaamini litarudi tu.”

Alipoulizwa kama wameripoti kwenye mamlaka husika baada ya taji hilo kupotea, alijibu: “Sisi tunajua tutalipataje, tunaamini litapatikana tu, tusizungumze mengi kwani Yanga pia ni mamlaka.”

NGA 04

WASIKIE TFF

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, kombe hilo likishakabidhiwa kwa mshindi linakuwa mali ya wahusika, halirudishwi.

“Kuhusu kupotea kwa Kombe la Yanga, hilo sisi hatuhusiki kabisa kufuatilia kwa sababu kila kitu tunachotoa kwa mshindi huwa ni mali yake wala hakuna maswala ya kurudisha,” alisema Ndimbo.

Yanga imebeba Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo, ikianza 2024 baada ya kuichapa Azam mabao 4-1, kisha 2025 ikaitandika Simba bao 1-0.