Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nenda Dhaira, mwambie Mafisango siyo freshi

Marehemu Abel Dhaira

Muktasari:

YULE kipa mrefu wa Uganda aliyeidakia Simba ikatoka sare mabao 3-3 na Yanga pale Taifa msimu wa 2013 ametangulia mbele za haki. Hii mechi ilichezwa siku chache kabla ya Jamal Malinzi hajapewa majukumu ya kuongoza mpira wetu.

YULE kipa mrefu wa Uganda aliyeidakia Simba ikatoka sare mabao 3-3 na Yanga pale Taifa msimu wa 2013 ametangulia mbele za haki. Hii mechi ilichezwa siku chache kabla ya Jamal Malinzi hajapewa majukumu ya kuongoza mpira wetu.

Abel Dhaira amemfuata yule kiungo machachari wa Simba,Patrick Mafisango aliyefariki mwaka 2012. Dhaira ameondoka ikiwa zimebaki wiki chache tu mwezi Mei tukumbuke miaka minne ya Mafisango kaburini na kuiachia Simba pia majonzi ambayo hayasahauliki. Kansa ya tumbo imemuondoa Dhaira mapema sana, hajaishi hata makumi matatu tangu aione duniani. Ameondoka bila hata ya kutusalia sala la mwisho kwenye ile Bibilia yake, lakini mwambie Mafisango Simba waliiona miguu yako ni mirefu mno wakakutuma Ulaya ukamalizie mpira wako.

Dhaira nenda kaka, nenda kapumzike kwa amani, urefu wako ulikaribia kuzidi mitambaa ya goli. Vicent na Manyika pale Simba wanatamani ungewaachia japo mikono yako wamzingue Ngoma na Tambwe, wanawafunga kwa kejeli mpaka imekuwa kero huku uswahili. Barthez naye alitamani umwambie jinsi ya kuwatuliza wale Ahly maana presha imempanda kwelikweli.

Miaka 28 uliyoishi hapa duniani ilikuwa michache sana lakini utakumbukwa kwa mengi. Express na URA za Uganda zinaikumbuka mikono yako mikubwa na umahiri wako wa kuzuia mashuti na mikwaju ya penalti ambazo pale Yanga bado ni tatizo sugu. AS Vita ya Kongo inahuzunika kupotea kwa wepesi wako golini, inakumbuka namna ulivyokuwa ukiambaa kutoka upande mmoja wa lango hadi mwingine.

Kuna wakati uliruka kama nyani na kusababisha kocha wa Uganda ‘The Cranes’, Milutin Sredojevic ‘Micho’ akuite katika kikosi chake tena na tena. Machozi yako yamebaki pia sambamba na nyota kadhaa wa IBV Iceland, wanaliona lango la timu yao kama limebaki wazi.

Miezi sita uliyokuwa ndani ya Simba haikuwa ya hasara, ulifanya mengi japo mabao mawili ya Mganda mwenzio, Hamis Kiiza na moja la Mrisho Ngassa yalitosha kukuchongea kwa mabosi wa Simba ambao walishuhudia timu yao ikitoka sare ya mabao 3-3 na Yanga mwaka 2013 na kuamua kukurejesha kwenu Uganda mapema.

Wakati mabosi wa Simba wakitafakari pengine kukurejesha tena klabuni hapo kama walivyowahi kufanya kwa Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Emmanuel Okwi na wengineo, wewe umeondoka, tena umeondoka mapema mno.

Nenda Dhaira, ukifika huko mwambie Patrick Mafisango aturudishie Simba ubingwa wetu. Mwambie medali ya ubingwa aliyovaa akiwa Simba ndiyo ya mwisho mpaka sasa, wengine wanajivunia za Mtani Jembe tu.

Mwambie kuwa wachezaji wa Simba siku hizi ndege wanaziona tu zikipita juu, mashindano ya kimataifa yamekuwa makubwa sana kwao. Tiketi aliyowaachia ndiyo iliyokuwa ya mwisho na mpaka sasa wameshindwa kupata tiketi nyingine. Mwambie hata kama ana bifu na sisi kwavile hatujarudi kupalilia kaburi lake pale Kinshasa, atusamehe tu mambo yamekuwa mengi halafu hapa Uwanja wa Ndege Dar na kwenyewe ukaguzi umekuwa mkali kwelikweli, hii ni awamu ya kazi tu hawataki watu wazurure hovyo. Ngosha kabana kwelikweli.

Mwambie bao alilofunga kwa mara ya mwisho pale Tanga dhidi ya Coastal Union limedumu kwa miaka mitano kabla ya Danny Lyanga na Hamis Kiiza kufanikiwa kuweka rekodi mpya msimu huu. Mueleze tu kwa upole, ataelewa Dhaira ila asikarike wewe kutemwa mwambie ulikumbuka sambusa za Iceland baada ya kuchoshwa na vitumbua vya pale Keko, ukaondoka.

Mweleze kabisa kuwa siku hizi Simba haiwezi tena kuifunga Yanga mabao 5-0, mwambie nyakati zimebadilika na sasa Simba inafungwa na Yanga mara mbili kwa msimu mmoja. Mwambie hata kama alisikia wakimpakazia kwamba alitaka kuwageuka asaini Yanga kabla hajafa wala asiweke rohoni aturudishie tu ubingwa wetu. Mwambie kuna kiungo mmoja anaitwa Justice Majabvi anajitahidi kuliziba lakini ni kama hapendwi sana ndani ya timu labda kwavile hapigi Cesto Laga na kucheza pulu pale Mango Gadeni.

Dhaira usimfiche kitu mwambie wachezaji aliocheza nao pale Simba wamebaki watatu tu. Mmoja ameanza kuwa bondia na anadaiwa kumpiga mwandishi wa Habari. Mwambie Mussa Hassan ‘Mgosi’ siku hizi hafungi tena amekuwa kocha mchezaji anasaidia kuwafunda vijana, anaipenda kazi yake sana kama alivyokuwa yeye.

Usisahau kumwambia kuwa Azam yake nayo imekuwa moto siku hizi. Haifungwi tena hovyo na Simba na Yanga. Mwambie imetwaa mataji ya Ligi Kuu na Kagame, inaogopwa kuliko ile APR, hata Simba wanaiogopa na wamegoma kucheza ligi mpaka imalize viporo vyake. Kabla hujatoa biblia yako kwenye kile kibegi cheusi mueleze kwamba Mrisho Ngassa sikuhizi anacheza Sauzi lakini wamempanga kwenye nafasi ya kiungo aliyokuwa anacheza yeye Simba imemshinda.

Nenda dhaira, nenda upumzike kwa amani. Ukimuona Steven Kanumba mwambie siku hizi Ray amekuwa mweupe, anasema anakunywa maji sana na ndiyo sababu amekuwa hivyo. Mweleze siku hizi Wema Sepetu hasomeki na Lulu ameendelea kuwa staa, anashinda tuzo hadi Nigeria.

Dhaira maisha yako Simba, hukuwa na wakati mzuri hukuwa kipa wa panga pangua lakini pumzika tu, mkumbushe Mafisango aturudishie taji, mwambie na vyombo vyake tumeshavipeleka Kinshasa.

Dhaira Februari 12 niliona uliandika ujumbe mrefu sana kwenye ukurasa wako wa Facebook ukataja mpaka hospitali na watu wote waliokuwa wakipambana kukusaidia kumbe ndio ulikuwa unatuaga na sisi.

Pumzika tu, hakuna jinsi huku presha zimetupanda wale Chad na wenyewe wamejitoa na pointi zetu zote zimefutwa inabidi tuanze upya, Uganda yako imefungwa ugenini. Lakini Mafisango najua atacheka kwavile DR Congo ilishinda. Ila tuache utani. Dhaira ulikuwa unajua kula sana, menyu yako haikuwa mchezo na ndio hivyo mchezaji anapaswa kula. Dhaira wakati wanaenda kukuzika pale Jinja natamani wasimame dakika chache pale Bugembe, uonje angalau wale kuku wa kuchoma wanaouzwa na wale dada waliovaa makoti ya bluu. Lakini kapumzike tu. Mwambie Mafisango atufikirie mwakani tunataka kupanda ndege mwanangu Jerry Muro anachonga sana, hatumezi kitu huku mtaani.

Anasikika yeye tu hata Mzee Akilimali haseimi kitu.