Mwambusi hana maisha marefu Yanga
WAZEE wa kudodosa wamepenyeza kuwa eti kocha mpya wa Yanga, Sebastien Migne anaweza kumpiga chini Juma Mwambusi mwishoni mwa msimu mara baada ya kuzoeana na wachezaji.
Chanzo kimoja cha ndani kimenipenyezea kuwa Migne amekubali kufanya kazi na Mwambusi kwa sababu ya uhitaji wake wa kuwasoma wachezaji mastaa na si vinginevyo.
Uoga wa Migne ni kuhujumiwa, hivyo anataka kuweka sawa mipango yake ili ahusike moja kwa moja mwenyewe, lakini hilo linaweza kubadilika kwa mujibu wa chanzo.