Ajibu kupigwa chini msimbazi
NYOTA wa Simba, Ibrahimu Ajibu huenda akaonyeshwa mlango wa kutokea mwishoni mwa msimu kama asipoonyesha mabadiliko yoyote, maana inaelezwa kiwango chake hakimvutii kocha wa timu hiyo, Didier Gomes.
Habari za ndani zinaeleza kuwa uamuzi huo unaweza kuwaumiza baadhi ya viongozi wa timu hiyo kutokana na mapenzi makubwa waliyonayo kwa mchezaji huyo.
Kuna kipindi Ajibu alisepa Simba na kwenda Yanga, baada ya kufanya vizuri huko na kupewa unahodha, vigogo hao inaelezwa walishinikiza kurejeshwa kwa mtoto wao huyo ambaye ni zao la timu ya vijana ya wekundu.