Musonye: Yanga bure kabisa
Musonye
Muktasari:
Cecafa waliamua kuiondoa Yanga katika michuano hiyo iliyoanza jana Ijumaa mjini Kigali, Rwanda baada ya kuwasilisha kikosi chenye wachezaji 13 kutoka kikosi chao cha vijana huku wachezaji wazoefu wakiwa saba pekee tena waliokuwa wakisugua benchi msimu uliopita.
Musonye azidi kukerwa na Yanga
MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye, amekerwa na kikosi alichokiita cha kipuuzi kilichopelekwa na Yanga kwenye michuano ya Kagame kabla hawajakipiga chini.
Cecafa waliamua kuiondoa Yanga katika michuano hiyo iliyoanza jana Ijumaa mjini Kigali, Rwanda baada ya kuwasilisha kikosi chenye wachezaji 13 kutoka kikosi chao cha vijana huku wachezaji wazoefu wakiwa saba pekee tena waliokuwa wakisugua benchi msimu uliopita.
Musonye aliwaambia waandishi wa habari mjini Kigali kwamba ilichofanya Yanga ni upuuzi.
“Yanga ya Tanzania wameamua kutuvuruga, kupuuza na kudharau michuano hii kwa kuleta kitimu cha hovyohovyo kisichokuwa na maana. Tumekataa tumesema tokeni na timu yenu, nendeni mkacheze popote pale mnapotaka huko kwenu Dar es Salaam.”
Kutokana na Yanga kutimuliwa, Azam imepewa nafasi.