Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msomeni Kayuni ana jambo lake!

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Leodgar Tenga amewataka makocha, wadau wa michezo kujiendeleza kielimu, kitaaluma katika michezo hasa soka ili kujijengea uwezo wa kushindana katika michezo kimataifa na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kasi.

Tenga ameyasema hayo wakati akizundua kitabu kiitwacho ‘Kocha wa Soka’ kilichoandikwa na mwalimu Sunday Kayuni huku akitoa rai kwa wapenzi wa soka na walimu kukitafuta kitabu hicho kwa kukisoma kwa faida zao binafsi na kwa maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

Katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, Tenga alimpongeza Kayuni kwa kuandika kitabu hicho na kusema amefanya kazi nzuri ya kuwaelimisaha walimu wa mpira wa miguu sio tu kuhusu mfumo wa njia ya ufundishaji, bali pia sifa na kazi za mwalimu wa mchezo wa mpira wa miguu.

“Pamoja na kuwa ni mpenzi wa mpira wa miguu lakini mimi ni mwalimu wa mpira wa miguu na muumini wa dhana kuwa ili mchezo huu uendelee hapa nchini tunahitaji kuuelewa na kujifunza mbinu za ufundishaji wake.

“Hivyo yaliyomo katika kitabu hiki siyo tu yatawawezesha walimu kufundisha vizuri zaidi bali pia kuwafahamisha wanastahili wawe na sifa zipi ili waheshimike na kuogeza ufanisi kiutendaji,” alisema Tenga.

Aliongeza “Maudhui ya kitabu hiki hayakulenga walimu peke yao, pia kimelenga kutoa elimu ya kiufundi ya mchezo wa mpira wa miguu kwa viongozi, wapenzi na wadau wa mchezo huu.

“Hapana shaka kuwa elimu ya kiufundi ya mpira wa miguu inakufanya uwe mdau na mshabiki bora zaidi kwa vile utakuwa na ufahamu mzuri zaidi wa nini kinaendelea, kujua matatizo ya timu yako hasa ni yapi na nini kifanyike.Uelewa wa mbinu za mchezo utamfanya mdau au mpenzi awe na ubishi wenye tija, yaani ubishi wa hoja na sio ubishi wa kinazi peke yake,” alisema.

Pia Tenga aliwataka viongozi kuwa na uelewa juu ya masuala ya msingi ya kiufundi ya mpira wa miguu kwani ndio njia pekee ya kuwafanya wawe na sifa ya kushika nafasi walizonazo na endapo kiongozi hana uelewa wa mambo muhimu ya msingi ya kiufundi basi hastahili kuongoza.

Naye mwandishi wa kitabu hicho, Kayuni alisema;

“Nimekuwa kocha kwa muda mrefu na nimepata bahati ya kufundisha katika timu ya Taifa ya vijana U 17, Taifa Stars, klabu mbalimbali zikiwemo za nje ya nchi na pia niliendelezwa kuwa mkufunzi wa hapa nyumbani na kimataifa hivyo nilipata uzoefu wa kutosha.”

Kayuni alisema kitabu hicho hususani ni kwa ajili ya makocha, kwani maudhui yaliyomo ni pamoja na historia ya mpira wa miguu, kocha ni nani,sifa za mtu kuwa kocha, kazi za kocha, Falsafa ya kocha, Maadili ya kocha, Saikolojia inamsaidia vipi kocha katika kazi yake, Habari ya Mawasiliano na namna bora ya ufundishaji wa mpira wa miguu

Naye mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alisema

“Ni kitu ambacho tulikipanga karibu miaka 20 iliyopita kwani ilikuwa tuandike kama chama cha makocha lakini hatukujipanga vizuri na mpaka sasa tumeshindwa lakini mwenzetu kaonyesha njia na ndio maana katika kusapoti kwenye dibaji mimi nimo na nimeweka sahihi.”