Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpira wa Simba na Yanga na uungwana wa fedha-2

Muktasari:

  • Haishangazi kwamba hata mipango ya kifedha hutegemea nani yuko madarakani na ni ya muda mfupi, fedha kwa wachezaji wa zamani hupatikana kama zawadi baada ya ushindi na si katika maandalizi ya ushindi.

WIKI iliyopita katika sehemu ya kwanza tuliona jinsi mambo yanavyoendeshwa kwenye ligi yetu na hali ya fedha kwenye klabu, endelea na sehemu ya pili...

SIMBA NA YANGA

Yanga na Simba ni klabu ngumu kuzielewa au kusoma mfumo wake wa kifedha na utawala na sababu kubwa na huenda ndiyo sababu inayozifanya klabu hizi zenye miaka zaidi ya 75 kutokusonga mbele ni kutokuwepo kwa uendelevu (sustainability/consistency).

Ni ngumu kuchambua uchumi na mfumo wa kifedha wa klabu hizi, na hata wanachama wake ni kama wanakuwa na homa za vipindi.

Mbaya zaidi ni kwamba wale wanachama wenye uwezo kifedha huwa tayari kusaidia wakati timu inafanya vizuri, ikiteleza kidogo huikimbia na hivyo uchumi wake kushuka na morali ya wachezaji kuwa chini. Lakini cha hatari zaidi ni kwamba kwa vilabu hivi vinavyotegemea wanachama wakati mwingine ni vigumu kwa uongozi kuwashirikisha au kuwaridhisha wanachama wote. Hali kama hii inapojitokeza baadhi ya wanachama wanaweza kuhujumu mipango ya klabu.

Kwa sura hii ni kwamba klabu hizi mafanikio yake hutegemea nani yuko madarakani au nini kinaendelea kwenye klabu. Haishangazi kwamba hata mipango ya kifedha hutegemea nani yuko madarakani na ni ya muda mfupi, fedha kwa wachezaji wa zamani hupatikana kama zawadi baada ya ushindi na si katika maandalizi ya ushindi.

Juhudi na fedha nyingi huelekezwa kwa wachezaji wapya au wale wa zamani ambao mikataba inakwisha na bado ni lulu klabuni.

Ieleweke wazi kwamba zaidi ya nusu ya bajeti ya klabu hizi hugharimiwa na mifuko binafsi. Mara chache sana fedha za usajili kutoka kwenye akaunti ya klabu na ndiyo maana haishangazi kuona picha magazetini na kwenye mitandao mchezaji akianguka sahihi na mezani zikiwepo burungutu za noti (kali ya Tanzania pekee)

Hata hivyo, kuingia kwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika udhamini wa klabu hizi kulileta chanzo cha uhakika (ingawa haitoshi kwa mahitaji yote) cha uendeshaji wa klabu hizi mbili. Vilevile udhamini huu ulikuja na masharti ya klabu hizi kujiendesha kiweledi kwa kutumia sekretarieti ambazo zipo hata kama hazipewi nafasi iliyokusudiwa na wadhamini na Azimio la Bagamoyo ili kuhakikisha udhamini unakuwa na tija.

Katika mkataba wa kwanza wa mwaka 2009 klabu hizi kwa pamoja zililamba Sh3 bilioni. Mwezi Agosti 2011 ukasainiwa mkataba wa miaka mitano, klabu kwa pamoja zinapata Sh5 bilioni kwa kipindi hicho na fedha hizo ni kwa ajili ya gharama ya udhamini, vifaa, usafiri, mikutano mikuu, ukarabati wa ofisi na fedha za ushindi ambazo bingwa hupewa Sh25 milioni na mshindi wa pili Sh15 milioni (Simba kwa kushika nafasi ya tatu wataikosa Sh5 milioni).

Udhamini wa TBL, mkataba na Push Media si haba kwa klabu hizi. (Kumbuka Yanga ina mkataba mwingine ambao kama haujaisha utakuwa unaelekea ukingoni). Lakini yote kwa yote, udhamini huu unawaongezea kifua kiasi kwamba klabu hizi hazikumbani na adha kama ya usafiri au kutokuwa na vifaa. Hata hivyo kama tutakavyoona uko mbele, bado matumizi, mahitaji na matarajio ya klabu hivi ni mara 1000 ya uwezo wake halisi.

Baada ya kufanya vibaya msimu uliopita, Yanga walichukua nafasi ya kuwa na uongozi mpya kuwapita wapinzani wao Simba. Yanga waliwapiku Simba katika usajili wa Mbuyu Twite na Kelvin Yondani ambao waliimarisha safu ya ulinzi iliyohitaji kuimarishwa.

Kwa kiasi kikubwa walijua wakati gani wa kucheza karata zao na kuziweka karibu na kifua na uongozi mpya ambao kwa kiasi kikubwa uko chini ya wafanyabiashara ulikuwa tayari kutumia juhudi binafsi pale mifuko ya klabu inapokuwa vibaya.

Tutake tusitake, viingilio vya milangoni bado ni muhimu kwa klabu za Tanzania. Yanga ilikuwa na mapato makubwa kuliko klabu nyingine yoyote kila ilipocheza kwenye Uwanja wa Taifa na mashabiki wa Yanga wana tabia ya kufurika uwanjani timu yao inapocheza hivyo kuiwezesha kupata mgawo mkubwa kuliko klabu nyingine.

Kwa jumla, Yanga haikuwa vibaya kifedha msimu uliopita hivyo haishangazi kwamba imechukua ubingwa. Simba ilikuwa na msimu mzuri 2011/12.

Ilikuwa kwenye mashindano ya kimataifa kwa muda mrefu na ilikuwa na dalili za kuendelea mbele zaidi lakini ilijifunga bao kwa kumpoteza Yondani na kama nilivyosema hapo juu hii ni matokeo ya klabu kutojali au kutimiza ahadi kwa wachezaji waliokwishasaini.

Kabla ya msimu kuanza klabu ikaboronga kwa kuchukua wachezaji wa kigeni bila kuwajua au kuwa na uhakika na uwezo wao (bahati mbaya au makusudi). Pesa nyingi ilipotea kuwafidia kina Kanu Mbiyavanga na wenzake ambazo zingeweza kumbakiza Yondani.

Itaendelea..

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga