Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpango apendekezwa Makamu wa Rais

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais.

Samia ampendekeza Dk Mpango kuwa Makamu wa Rais

Jina la Mpango limesomwa bungeni mjini Dodoma leo Jumanne Machi 30, 2021 na Spika Job Ndugai aliyeletewa bahasha yenye jina hilo na mpambe wa kiongozi mkuu huyo wa nchi.

Jina la Dk Mpango liliwekwa katika bahasha mbili ya juu ilikuwa ya kaki na ya ndani ilikuwa nyeupe, Spika Ndugai alianza kusoma nyaraka hiyo ya rais akirudia rudia maneno ya utangulizi kabla ya kulisoma jina.

Baada ya kusoma jina wabunge walishangilia kwa nguvu  huku Dk Mpango akionekana kushikwa na butwaa huku  wabunge wakinyanyuka kwenye viti vyao na kumfuata kumpongeza.


HABARI ZAIDI ZITAKUJIA HAPA HIVI PUNDE...