Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Michuano ya Cecafa kuanza leo Rwanda

CECAFA Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia tamati Agosti 31, 2026, Tanzania Bara inawakilishwa na Simba Queens, huku Mafunzo SC ikishiriki kwa mara yao ya kwanza kutokea Zanzibar.

MASHINDANO ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake yanaanza leo Ijumaa Agosti 21, jijini Kigali, Rwanda, huku Yei Joint Stars ya Sudan Kusini ikikipiga na Denden FC ya Eritrea mechi ya Kundi A.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kufikia tamati Agosti 31, 2026, Tanzania Bara inawakilishwa na Simba Queens, huku Mafunzo SC ikishiriki kwa mara yao ya kwanza kutokea Zanzibar.

Mechi hiyo itapigwa Uwanja wa Kigali Pele kuanzia saa saba mchana, kwa saa za Afrika Mashariki, ikiwa ni ya kwanza ya mashindano hayo yanayoshirikisha timu 10.

mehi nyingine ya kundi hilo Rayon Sports ya Rwanda itakipiga na Mafunzo SC ya Zanzibar, uwanjani hapo saa 10 jioni.

Yei Joint Stars inashiriki mashindano hayo ikiwa mara ya sita lakini haikuwahi kucheza fainali, jambo linaloipa uzoefu mkubwa wa mashindano ya ukanda.

Timu hiyo inaingia kwenye mechi hiyo na jukumu la kuanza kwa matokeo mazuri dhidi ya Denden ambayo ni mara yao ya pili katika mashindano haya baada ya kufanya hivyo mwaka 2025, Nairobi, Kenya, lakini haikuvuka hatua ya makundi.

Yei Joint Stars inafahamu umuhimu wa kupata pointi katika mechi ya kwanza kutokana na mfumo wa mashindano ulivyo. Kundi A lina timu nne ambazo ni Rayon Sports ya Rwanda, Yei Joint Stars, Mafunzo ya Zanzibar na Denden FC na ni mbili zilizomaliza kileleni zikifuzu nusu fainali.

Rayon Sports si mgeni kwenye mashindano hayo. Mwaka 2025 ilifika hadi fainali ilipokutana na JKT Queens ya Tanzania katika mechi ya kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika ikaondolewa kwa kuchapwa bao 1-0, Wanajeshi hao walinyakua taji hilo.

Timu hiyo inahitaji kuanza kwa ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri mapema kabla ya kukutana na Yei Joint Stars na Denden katika michezo inayofuata.

Kwa upande wa Mafunzo, uwakilishi wa Zanzibar kwenye mashindano hayo unaifanya mechi hiyo kuwa muhimu si kwa timu pekee bali pia kwa soka la wanawake Zanzibar. Mafunzo ipo kundi lenye timu nne na itahitaji kuanza kwa matokeo mazuri ili kujiweka vizuri dhidi ya wapinzani wake. Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo mshambuliaji wa Mafunzo, Zainab Dotto, amesema wanafahamu ugumu wa kukutana na timu zinazokuwa mwenyeji hivyo watapambana kuhakikisha walichoelekezwa na makocha kinafanyiwa kazi.

“Tunajua ni mechi ngumu sana kwa sababu hii ni mara yetu ya kwanza kucheza michuano hii lakini tunaamini kwa maandalizi tuliyoyafanya tutafanya vizuri.”