Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mhilu anaitamani tano bora Ligi Kuu Bara

MHILU Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa Mhilu amefunga mabao mawili, akiwa na kazi kubwa ya kufanya kuiongoza Geita Gold akiwa nahodha.

MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, Yusufu Mhilu, amesema japokuwa Ligi Kuu Bara msimu huu ni ngumu na ushindani upo wa hali ya juu, lakini anatamani kumaliza akiwa kwenye tano bora ya wafungaji wa mabao mengi.

Hadi sasa Mhilu amefunga mabao mawili, akiwa na kazi kubwa ya kufanya kuiongoza Geita Gold akiwa nahodha.

Mshambuliaji huyo msimu uliopita wa 2025-2026 Geita Gold ikiwa Ligi ya Championship, alifunga mabao matano akiisaidia timu hiyo kurejea Ligi Kuu Bara, jambo ambalo amesema linampa nguvu ya kupambana kuhakikisha anatimiza malengo yake.

“Binafsi ugumu wa ligi nauchukulia kama chachu ya kujituma zaidi, kuanzia ushindani wa namba katika timu hadi mechi dhidi ya wapinzani wetu, hilo litanisaidia kufikia malengo yangu ya kutamani kumaliza na mabao mengi,” amesema Mhilu na kuongeza;

“Msimu uliopita tulikuwa Championship, hivyo kurejea kwenye Ligi Kuu kama mchezaji, lazima nifanye kitu cha kunitambulisha ujio wangu.”

Mshambuliaji huyo amekuwa na mwendo wa kupanda na kushuka katika ufungaji ndani ya Ligi Kuu Bara na msimu 2018-2019 alimaliza na mabao 13, kisha 2019-20 (tisa), baada ya kusajiliwa Simba 2020-2021 alifunga mabao mawili kwenye Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na aliporejea Kagera kwa mkopo 2022 alifunga bao moja, jambo alilosisitiza anatamani kurejesha heshima ya kucheka na nyavu.

“Kwangu ni suala la muda kuonyesha kwa matendo, kikubwa nafanya mazoezi kwa bidii, napumzika ili kuhakikisha mwili wangu unapata nguvu ya kupambana zaidi,” amesema.