Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Geita Gold amtaja Chirwa

CHIRWA Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Maulid amesema kucheza na Chirwa katika timu moja kumemwongezea nafasi ya kuendelea kujifunza zaidi kutokana na uzoefu wake, japo licha ya ushindani ila ataendelea kufanya vizuri kila atakapopata nafasi kikosini.

MSHAMBULIAJI wa Geita Gold, Maulid Shaban amesema kucheza timu moja na Mzambia Obrey Chirwa ni jambo nzuri ndani ya kikosi hicho, ingawa ni changamoto pia kwake, kutokana na ushindani wa nafasi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Maulid amesema kucheza na Chirwa katika timu moja kumemwongezea nafasi ya kuendelea kujifunza zaidi kutokana na uzoefu wake, japo licha ya ushindani ila ataendelea kufanya vizuri kila atakapopata nafasi kikosini.

"Watu wanapaswa kutambua kucheza Championship ni tofauti na Ligi Kuu Bara, ndiyo maana baada ya timu kuipandisha uongozi ulifanya usajili mwingine wa kuongeza washambuliaji bora kwa lengo la kuendana na ushindani uliopo," amesema Maulid.

GEIT 01

Aidha, mshambuliaji huyo amesema uwepo wa washambuliaji wengine pia ambao ni Yusuph Mhilu na Mkongomani Fabrice Ngoy, ni ishara nyingine ya kuonyesha ushindani katika eneo hilo, jambo ambalo linabakia kwa mchezaji mwenyewe kujituma zaidi.

"Msimu uliopita kulikuwa na ushindani wa nafasi ya kucheza lakini siyo kama sasa, kwangu ni fursa ya kujituma ili kazi ibakie kwa benchi la ufundi, nafurahia sana uwepo wa wenzangu kwa sababu wanapofanya vizuri nazidi kujifunza," amesema.

Maulid ni mfungaji bora wa Championship msimu wa 2025-2026, baada ya kufunga mabao 18 akiwa na Geita Gold na idadi hiyo ni sawa na ya Chirwa wakati akicheza Kagera Sugar. Kwa sasa wachezaji hao wote wameungana tena.

GEIT 02

Chirwa aliyetamba na timu mbalimbali Tanzania zikiwemo, Yanga, Azam FC, Namungo FC, KenGold na Kagera Sugar, amekuwa na mwenendo mzuri na wa kuvutia na kikosi hicho cha Geita Gold, kwani hadi sasa amekifungia mabao manne ya Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wa Maulid ambaye bado hajapata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi hicho kinachofundishwa na Kocha Mkuu, Zubery Katwila, bado hajafunga bado.

Maulid alijiunga na Geita Gold, Septemba 11, 2025, akitokea Coastal Union, ambayo msimu wa 2024-2025, aliifungia mabao mawili ya Ligi Kuu, huku bao la mwisho alilifunga katika sare ya kikosi hicho ya 1-1 dhidi ya KMC FC, Desemba 29, 2024.