Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi vs Ronaldo : Messi ajikatia tamaa, Maradona amkingia kifua

Muktasari:

Gazeti maarufu la Ole lilikwenda mbali zaidi kwa kumtaka Messi ajivue unahodha wa timu hiyo na kama ilivyo ada Maradona naye akawa na cha kusema

TOLEO lililopita, mwandishi, Luca Caioli alizichambua shutuma alizokumbana nazo Messi baada ya Argentina kukwama kwenye fainali za Kombe la Dunia Brazil mwaka 2014 na Copa America 2015 huku Maradona naye akiongoza madongo ingawa baadaye alionekana kumtetea Messi. Sasa endelea…

Gazeti maarufu la Ole lilikwenda mbali zaidi kwa kumtaka Messi ajivue unahodha wa timu hiyo na kama ilivyo ada Maradona naye akawa na cha kusema,

“Tuna mwanasoka bora duniani, ambaye anakwenda kufunga magoli manne dhidi ya Real Madrid. Huyo huyo anakuwa wa kuzungukazunguka na kuugusa mpira mara chache. Niambie wewe ni Muargentina au Msweden?

Hata hivyo, baadaye Maradona ni kama alichoshwa na mambo ya Messi akahitaji apewe utulivu aliposema, “Messi anatakiwa kuchukuliwa kama mchezaji mwingine ambaye anavaa jezi ya timu ya Taifa, ndio yeye ni mchezaji bora duniani, kwa mazuri au mabaya lakini sikilizeni hajaua mtu, hajabaka mtu tusigeuze hii kama michezo ya kuigiza majukwaani.

Kitu ambacho pengine hakuna ambaye angeweza kukifikiri katika timu ya Argentina, ni haikupita miezi 12 baadaye, Messi akajikuta akishushiwa lawama kwa mara nyingine.

Messi hakuwahi kuficha ukweli ndoto yake kubwa imekuwa ni kubeba taji na timu ya Argentina,

“Naweza kubadilishana mataji matano ya Ballon d’Or na Kombe la Dunia, ni wazi taji la timu ni muhimu sana na kushinda Kombe la Dunia ni mafanikio makubwa kwa mchezaji yeyote,’’ alisema.

Akawa na nafasi nyingine ya kutimiza ndoto zake mwaka 2016 wakati wa michuano ya Centennial Copa America mwaka 2016 nchini Marekani.

Halikuwa Kombe la Dunia lakini ni mashindano muhimu kiasi chake ambayo yangeweza kumpoza.

Katika hatua ya kwanza, Messi aliiongoza timu imara ambayo haikuwa na tatizo la kuwaangamiza wapinzani wake Chile kwa mabao 2-1, Panama mabao 5-0 huku Messi akipiga hat trick na Bolivia kwa mabao 3-0.

Messi aliikosa mechi ya ufunguzi na hakucheza kwa dakika zote 90 lakini uwepo wake ulijidhihirisha kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Katika robo fainali waliigaragaza Venezuela mabao 4-1 na kukata tiketi ya nusu fainali ambako walikutana na Marekani mwenyeji wa mashindano na kumchapa mabao 4-0.

Kama zali vile kikosi kilichocheza mechi ya fainali ya Juni 27 kikawa kile kile kilichocheza fainali ya mwaka uliopita; Argentina na Chile, kila kitu kilichozungumzwa kikawa ni kuhusu matokeo tofauti safari hii hadi bahati ilipokwenda mahali pake.

Messi, mshambuliaji wa Barca akajitolea uwanjani kikamilifu, lakini wachezaji wanzake wakapoteza nafasi tatu za kupata mabao na hadi filimbi ya kumaliza mchezo inapulizwa matokeo yalikuwa 0-0 na bado hakukuwa na bao lolote hata katika dakika 30 za nyongeza.

Kwa mara nyingine tena hatima ya Argentina na Chile ikawa kwenye mikwaju ya penalti, na kwa mara nyingine Argentina inarudi nyumbani mikono mitupu.

Safari hii, Messi akakosa mkwaju wake wa penalti akaanguka chini akiwa mwenye kulia, dakika chache baadaye akiwa katika eneo la mikutano ya habari akatangaza kuachana na timu ya Taifa bila ya kusita.

“Huu ni wakati mgumu kwangu, ni ngumu kuelezea, nikiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo niliona sasa imetosha, mwisho umefika kwa upande wangu na timu ya Taifa, hicho ndicho ninachokiona kwa sasa, ni huzuni kubwa kwamba hili limeendelea kutokea, nimekosa penalti muhimu.

“Hali ndiyo hiyo hilo ni bora kwa kila mmoja wetu, hatuwezi kuridhika kwa kufikia fainali na tusiwe washindi, nimepambana kwa wakati wangu na kujaribu mara nyingi ili niwe bingwa na Argentina haikuwezekana, sitoweza kufanya hivyo.

Baada ya kushindwa fainali nne (mwaka 2007, 2015 na 2016 Copa America na Kombe la Dunia 2014), Lionel ni kama alijikatia tamaa, aliamua kukubali yaishe, na kustaafu kuichezea timu ya Taifa ya Argentina.

Itaendelea Jumanne ijayo