Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi moja tu, Wembe yaachana na kocha

KINYONGE Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo alifanikiwa kuionoa timu hiyo kwa mchezo mmoja wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) dhidi ya Uhamiaji ambao walipokea kichapo cha bao 1-0.

TIMU ya Wembe iliyopanda daraja msimu huu kushiriki Ligi Kuu Zanzibar, imeachana na kocha wake mkuu, Juma Pweka chanzo cha uamuzi huo bado hakijafahamika.


Kocha huyo alifanikiwa kuionoa timu hiyo kwa mchezo mmoja wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) dhidi ya Uhamiaji ambao walipokea kichapo cha bao 1-0.

Licha ya Wembe kutoweka wazi sababu za kuachana na kocha huyo, Mwanaspoti linatambua kuwa kulitokea sintofahamu baina yake na uongozi. Inaelezwa kwamba, kocha huyo alihitaji mmoja wa wachezaji kikosini hapo kuondolewa, na kama haitafanyika hivyo, basi yeye ataondoka.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Wembe, Hamed Hemed, amekiri timu hiyo kuachana na kocha huyo, huku akiwa hayupo tayari kuweka wazi sababu za kufanya hivyo.

“Hizo taarifa za kuachana na aliyekuwa kocha mkuu ni kweli na tayari nafasi yake ilishapata mtu wa kuiziba tangu mechi kati yetu na Black Sailors,” amesema.

Mkurugenzi huyo amesema hawezi kutoa ufafanuzi wa hilo kwani halipo chini yake na anachotaka kieleweke ni kuwa Wembe imeachana na kocha huyo.

Juma amekuwa kocha wa kwanza kuondolewa kuondolewa katika Ligi Kuu Zanzibar tangu msimu huu wa 2026-2027 uanze Agosti 29, 2026.

Baada ya Wembe kuachana na Juma, kikosi hicho mechi iliyofuatia dhidi ya Black Sailors, iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.