Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MCL ilivyoshiriki tuzo ya Mwajiri bora wa Mwaka 2023

Tuzo ya ukuzaji na vipaji ni miongoni mwa tuzo 14 zilitolewa katika hafla ya kuwatambua washindi wa tuzo ya Mwajiri bora wa mwaka (EYA) zilizotolewa leo Desemba 4 jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo, tuzo 14 zilitolewa kwenye vipengele tofauti, ikaishindanisha kampuni mbalimbali ikiwamo ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ambayo iliingia kwenye kinyang'anyiro ikiwania tuzo mbili katika kipengele cha utofautishwaji na ushirikishwa na ile ya Usawa wa Kijinsia na usawa katika maeneo ya kazi.

Mwananchi iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bakari Machumu na viongozi wengine ilishindwa kutetea tuzo ya Usawa wa Kijinsia na usawa katika maeneo ya kazi ambayo imechukuliwa na NMB na ile ya Utofautishwaji na ushirikishwa ambayo iliwania kwa mara ya kwanza ambayo imechukuliwa na CCBRT.

Awali, Meneja Rasilimali watu wa MCL, Paul Hamidu alisema mwaka jana kampuni hiyo ilishinda tuzo ya Usawa wa Kijinsia na usawa katika maeneo ya kazi ambayo iliwapa morali ya kuwania kwa mara nyingine mwaka huu na kuingia kwenye fainali katika kipengele hicho.

"Vilevile tuliingia kwenye fainali katika kipengele kingine cha Utofautishwaji na Ushirikishwa, ambavyo kama kampuni tumekuwa na mazingira mazuri zaidi katika maeneo hayo na mengine mengi kwa wafanyakazi," alisema.

Katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kampuni ya Barick North Mara iliibuka mshindi wa jumla na kutwaa Tuzo ya Mwajiri bora wa mwaka (EYA) 2023.

Akikabidhi tuzo hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, ajira, vijana na watu wenye ulemavu, profesa Joyce Ndalichako aliyemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema tuzo hizo zinaleta maendeleo na ustawi kwa wafanyakazi.

"Serikali inatambua mchango wa waajiri na chama cha ATE ambayo imechangia kutatua changamoto za waajili na wafanyakazi," alisema.

Alisisitiza ATE kuongeza kipengele cha malengo ya 03 katika kutokomeza ukimwi.

"Waajili muwe na msukumo wa pamoja katika mapambano ya ukimwi na virusi vya ukimwi, endeleeni kutokomeza unyanyapaa na kuwahamasisha wafanyakazi kupima kwa hiari," alisema Profesa Ndalichako kwa niaba ya waziri mkuu.

Alisema waajiri waweke mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu katika mazingira ya kazi.

Katika hafla hiyo, tuzo 14 zilitolewa kwenye vipengele tofauti huku, Mkurugenzi wa MCL, Bakari Machumu akikabidhi tuzo ya "best small organization" ambayo ilichukuliwa kampuni ya East West Seed Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Suzanne Ndomba-Doran alisema ushiriki wa kampuni kwenye tuzo hizo unadhihirisha namna wanavyothamini wafanyakazi na wamedhamiria kuboresha utendaji kazi na usimamizi wa rasilimali watu katika maeneo yao ya kazi.