Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbili za kibabe Ligi Kuu Bara

Muktasari:

  • Fountain Gate inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kazi ya kusahihisha kilichotokea kwenye raundi ya kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0 na Singida Black Stars, Agosti 14, 2026, huku Mashujaa ikitoka kushinda dhidi ya Coastl Union kwa bao 1-0 kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

LIGI Kuu Bara inaendelea leo Jumanne, Agosti 18, 2026, kwa mechi mbili kupigwa ambapo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Fountain Gate itaikaribisha Mashujaa, huku Namungo ikiwa mweyeji wa Geita Gold, mechi itakayopigwa Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Fountain Gate inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kazi ya kusahihisha kilichotokea kwenye raundi ya kwanza baada ya kufungwa mabao 3-0 na Singida Black Stars, Agosti 14, 2026, huku Mashujaa ikitoka kushinda dhidi ya Coastl Union kwa bao 1-0 kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kwenye mechi tano zilizokutana timu hizo, Mashujaa inaonekana kuwa na rekodi nzuri zaidi dhidi ya Fountain Gate, ikiwa imeshinda mbili, huku Fountain Gate ikiwa haijawahi kushinda na michezo mitatu ikimalizika kwa sare. Mashujaa ilishinda 1-0 katika mchezo wa mwisho Juni 24, 2026,  kabla ya Aprili 5, 2025 kuondoka na ushindi wa mabao 3-0, na michezo mingine mitatu ikiisha kwa sare ya 1-1, 2-2 na 0-0.

Rekodi zinaonyesha Fountain Gate haijawahi kushinda kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Mashujaa, mara ya mwisho Mashujaa iliondoka na ushindi wa bao 1-0, Juni 24, 2026.

Katika mechi hizo, Fountain Gate ilifunga mabao matatu dhidi ya saba ya wapinzani wake. Hilo linaifanya mechi hiyo kuwa nafasi kwa Fountain Gate kulipa kisasi cha kipigo cha mwisho, wakati Mashujaa ikitaka kuendeleza ubabe wake wa hivi karibuni dhidi ya wenyeji hao.

Kule Lindi nako kutakuwa na vita nyingine baada ya Namungo kuanza msimu kwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga, kwenye Uwanja wa Majaliwa, huku Geita Gold yenyewe ikianza kwa ushindi wa 1-0 mbele ya Mbeya City.

Katika mechi sita zilipokutana timu hizo, Namungo imeshinda tatu, Geita Gold mbili, huku mchezo mmoja ukimalizika kwa sare. Namungo ilianza kushinda 2-0 (Septemba 27, 2021), ikashinda tena 2-1 (Februari 26, 20223) na ushindi wa 2-0 (Mei 10, 2024).

Geita Gold ilipata ushindi wa 2-1 (Oktoba 22, 2022) na 1-0 (Novemba 26, 2023), wakati mchezo wa Februari 25, 2022 ukimalizika kwa sare ya 1-1.

Hata hivyo kwenye ushindi wa mechi hizo sita rekodi zinaibeba Namungo mbele ya Geita Gold. Namungo ikiwa mwenyeji, imecheza mechi tatu na imeshinda zote tatu, Namungo 2-0 Geita Gold (Mei 10, 2024), Namungo 2-1 Geita Gold (Februari 26, 2023) na Namungo 2-0 Geita Gold (Septemba 27, 2021).