Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coastal ilivyoinasa saini ya kipa JKU aliyehitajika Simba

Muktasari:

  • Kabla ya kumwaga wino kwa Wagosi wa Kaya, kipa huyo alikuwa akihitajika na Simba ambapo alifika hadi kambini na kukaa kwa takribani siku tatu, lakini dakika za mwisho akaibukia Coastal Union.

ALIYEKUWA kipa namba moja wa timu ya JKU, Ahmed Issa, tayari amejiunga na Coastal Union kwa ajili ya kuongeza nguvu golini kwa msimu wa 2026-2027, huku ikibainika namna klabu hiyo ilivyofanikiwa kuinasa saini yake.

Kabla ya kumwaga wino kwa Wagosi wa Kaya, kipa huyo alikuwa akihitajika na Simba ambapo alifika hadi kambini na kukaa kwa takribani siku tatu, lakini dakika za mwisho akaibukia Coastal Union.

Inadaiwa kuwa, viongozi wa Simba walishindwa kumalizana na JKU ambayo ilikuwa na mkataba na kipa huyo wa miaka miwili aliousaini wiki chache kabla ya kuhitajika na Simba.

Mtu wa karibu na kipa huyo, aliliambia Mwanaspoti kwamba, mazungumzo ya Simba na JKU hayakukamilika, ndiyo maana dili hilo likaishia njiani, ndipo Coastal Union ikaingilia kati na kufanya biashara kufuatia mazungumzo yao kwenda vizuri.

Akizungumza na Mwanaspoti, kipa huyo alisema kwasasa yeye ni mchezaji halali wa Coastal Union kwani ameshasaini mkataba na yupo kambini akiendelea na mazoezi kujiandaa na mechi zijazo.

“Mimi kwasasa ni mchezaji wa Coastal Union, nimeshasaini mkataba na nipo kambini naendelea na mazoezi,” alisema kipa huyo.

Kipa huyo alisema anafurahia kuanza safari ya kuichezea Ligi Kuu Bara kwani hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yake ya muda mrefu.

Alisema zipo timu nyingi za Zanzibar zilizokuwa zinahitaji huduma yake, lakini aliamua kuvumilia kubaki JKU ili kutimiza ndoto yake ya kucheza Tanzania Bara na hilo limefanikiwa.

Katika msimu uliopita wa 2025-2026, Issa kwenye Ligi Kuu Zanzibar, alimaliza nafasi ya pili kwa makipa wenye clean sheet nyingi akiwa nazo kumi, nyuma ya kinara, Hamad Ubwa aliyekuwa Mlandege na clean sheet 12.

Katika Kombe la Muungano mwaka 2025, Issa alikuwa kipa bora wa mashindano hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba ambapo Yanga ilitwaa ubingwa kwa kuifunga JKU.