Mashujaa yanasa wawili ikijipanga
Muktasari:
- Neema ambaye aliwahi kukipiga Yanga Princess sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa Queens kinachojiandaa na msimu mpya wa mashindano ya Ngao ya Jamii na ligi.
MASHUJAA Queens imeanza kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Wanawake Bara baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji Neema Charles Chibara, akitokea Fountain Gate Princess.
Neema ambaye aliwahi kukipiga Yanga Princess sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa Queens kinachojiandaa na msimu mpya wa mashindano ya Ngao ya Jamii na ligi.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuongeza ushindani mpya ndani ya kikosi cha Mashujaa Queens, ambacho kinaendelea kujipanga kwa ajili ya kukabiliana na ushindani wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania Bara.
Mbali na Neema, Mashujaa Queens imeongeza nguvu nyingine baada ya kumsajili aliyekuwa nyota wa Tausi FC, Yasinta Malimba, ambaye amejiunga na klabu hiyo kama mchezaji huru.
Yasinta amefikia hatua hiyo baada ya kumaliza mkataba wake na Tausi FC, hivyo na kuamua kuendelea na safari yake ya soka akiwa ndani ya kikosi cha Mashujaa Queens.
Ujio wa wachezaji hao wawili unaongeza chaguo kwa benchi la ufundi la Mashujaa Queens, huku klabu hiyo ikilenga kuwa na kikosi kitakachokuwa tayari kupambana katika msimu mpya wa ligi.
"Ukiangalia wachezaji wote wawili wana uzoefu kwenye ligi na wana vipaji vikubwa kwa hiyo msimu huu tumejipanga kuhakikisha tunakuwa na damu changa na wale wazoefu ili kuwa na kikosi chenye ngumu," kilisema chanzo hiko.