Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashujaa Queens yabeba kiungo Tausi FC

MASHUJAA Pict

Muktasari:

  • Ujio wa Yasinta unaongeza chaguo kwenye kikosi cha Mashujaa Queens, ambacho kinaendelea kujenga timu kuelekea msimu mpya wa ligi.

MASHUJAA Queens imeinasa saini ya aliyekuwa nyota wa Tausi FC, Yasinta Malimba kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Tausi FC mwishoni mwa msimu uliopita.

Ujio wa Yasinta unaongeza chaguo kwenye kikosi cha Mashujaa Queens, ambacho kinaendelea kujenga timu kuelekea msimu mpya wa ligi.

Mashujaa Queens imekuwa miongoni mwa timu zinazofanya maboresho ya kikosi kwa ajili ya msimu mpya, na usajili wa Yasinta ni sehemu ya hatua hizo za kukijenga kikosi chenye ushindani zaidi.

“Kwa ligi ilipofika inahitaji kuwa na wache zaji wa aina tofauti kwanza wale vijana ambao wataongeza nguvu na wale wenye uzoefu ndio maana sajili zetu zimelenga humo,” amesema mmoja wa viongozi wa timu hiyo.

Akiwa Tausi kiungo huyo alikuwa mchezaji muhimu na kuisadia timu hiyo kumaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa ni mara yake ya kwanza kucheza WPL.