Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Queens kumrejesha kipa Mashujaa

JKT Pict
JKT Pict

Muktasari:

  • Asha, ambaye anaifahamu vizuri klabu hiyo kutokana na kuitumikia hapo awali, anaweza kurejea JKT Queens kwa ajili ya  msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikiwa sehemu ya mipango ya kuimarisha nafasi ya ulinzi.

JKT Queens iko kwenye mpango wa kumrudisha kipa wake wa zamani, Asha Mrisho, ambaye msimu uliopita alikuwa kwenye kikosi cha Mashujaa Queens.

Asha, ambaye anaifahamu vizuri klabu hiyo kutokana na kuitumikia hapo awali, anaweza kurejea JKT Queens kwa ajili ya  msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikiwa sehemu ya mipango ya kuimarisha nafasi ya ulinzi.

Iwapo dili hilo litakamilika, Asha anatarajiwa kuwa chaguo muhimu katika kikosi cha JKT Queens, hasa katika kuongeza ushindani kwenye nafasi ya mlinda mlango na kutoa mbadala kwa kipa namba moja wa timu hiyo, Najiat Abas.

Uzoefu wa Asha akiwa Mashujaa Queens unaweza kuwa miongoni mwa vitu vinavyomfanya awe chaguo la JKT Queens,  ambayo tayari anaifahamu mazingira yake.

Kurejea kwa Asha JKT kunaweza kusaidia kuongeza kina cha kikosi kwa ajili ya msimu mpya, ikizingatiwa timu hiyo inaingia katika msimu ambao inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa katika mbio za ubingwa.

“Najat amekuwa akitumika muda mrefu kwenye timu ya taifa hadi klabu hivyo ndio maana tumemrejesha Asha ili aweze kumsaidia na apumzike kwenye baadhi ya mechi.”