Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Yanga wabishi

Muktasari:

  • Uwanja wa Manungu una uwezo wa kuingiza mashabiki 5000 na wasimamizi wa uwanja huo wamepanga kuingiza mashabiki 3000 leo.

MASHABIKI waliokuja kushuhudia mechi kati ya Mtibwa Sugar na Yanga walianza kufika kwenye uwanja wa Manungu kwa kusuasua baada ya mageti kufunguliwa saa 4:00 asubuhi.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili inatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni ambapo kuanzia saa 8 ndipo mashabiki walianza kufika kwa wingi na kuingia uwanjani wakitumia mageti yote mawili yaliyopo uwanjani hapa.

Mashabiki wa Yanga ndio walionekana kuwa wengi zaidi huku wengine wakiingia na vingoma vyao, wakiimba na kucheza.

Awali meneja wa uwanja huo Gedfrey Komba alisema mipango yao ni kuingiza mashabiki 3000 tu akitoa sababu kuwa mashabiki wa timu za Kariakoo Simba na Yanga wanakuwa na vurugu wakiruhusiwa kuingia wengi.

Ingawa meneja huyo amesisitiza idadi kutokuzidi lakini hadi sasa inaonekana kuzidi kutokana na wingi wa mashabiki walioingia na wale waliobaki nje ya uwanja wakiwa kwenye foleni ya kuingia.

Uwanja wa Manungu hauna majukwaa ya kukaa kwa ajili ya mashabiki bali mashabiki husimama huku kukiwa na jukwaa moja ambalo ni jukwaa kuu linalotumiwa na viongozi mbalimbali wa timu na wageni maalumu.