Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Simba, Yanga jino kwa jino Betika mtoko wa kibingwa

Mashabiki wa soka wa vigogo, Simba na Yanga wameanza kukoleza moto wa dabi ya Aprili 16 baada ya kila upande kupata mshindi kwenye droo ya kwanza ya Betika Mtoko wa Kibingwa.

Mashabiki hao, Bahame Masangwa Balele wa Simiyu  na Constantine Constantine Mbele wa Ruvuma wamefungua dimba la kuwa wa kwanza kuingia kwenye promosheni ya Mtoko wa Kibingwa inayoendeshwa na kampuni ya Betika nchini.

Februari 7, mwaka huu Kampuni hiyo ya kubashiri matokeo ilizindua promosheni ya tano ya Mtoko wa Kibingwa ambayo msimu huu inawagharamia mashabiki 100  kutoka maeneo mbalimbali nchini watakaoibuka washindi kwenye jackpoti mbalimbali za Betika kuishuhudia dabi hiyo yenye upinzani wa jadi.

Kampeni hiyo ya miezi miwili inawapa fursa mashabiki wa soka nchini kujishindia zawadi mbalimbali, kubwa kuliko ikiwa ni kwenda Dar es Salaam kushuhudia dabi hiyo laivu kwenye uwanja wa Mkapa, Aprili 16 gharama zote zikiwa chini ya Betika.

Washindi wa droo ya kwanza kwa nyakati tofauti wamesema hiyo ni mara yao ya kwanza kupata fursa ya kuishuhudia dabi laivu kwani wamekuwa wakiitizama miaka yote kwenye luninga.

"Sijawahi kufika Dar es Salaam, na sikuwa na ndoto hizo kwamba ipo siku nitakwenda kwa ajili ya kuishuhudia dabi, Betika walipozindua kampeni ya Mtoko wa Kibingwa, nilijaribu bahati yangu, sikuwa na matarajio ya kushinda kwani sijawahi kushinda, nashukuru msimu huu nimepata fursa hiyo,"alisema Balele na kuongeza.

"Natamani siku yenyewe ifike, nikaishuhudie Yanga ikikoleza kasi ya ubingwa kwa kumchinja mnyama, sina shaka na timu yangu ya Yanga katika dabi hiyo, naamini tunashinda," alisema shabiki huyo kindaki ndaki wa Yanga.

Constantine ambaye ni mnazi wa Simba yeye anaamini Aprili 16 wanakwenda kufuta 'uteja' kwa watani zao Yanga akimtaja Mosses Phiri kuwa ndiye mtu anayemtarajia apindue meza ya dabi hiyo.

"Haiwezekani Simba tufungwe na Yanga mfululizo mara tatu, hilo jambo haliwezi kutokea Aprili 16, nawashukuru Betika kwa kutoa fursa kwa mashabiki, ninachokisubiri ni siku tu ifike nikamshuhudie Mnyama akiunguruma kwa Mkapa," amesema.

Meneja Mkuu wa Betika Tanzania, Tumaini Maligana amesema washindi hao ni wa droo ya kwanza wa wiki iliyopita huku wale wa wiki hii wakitarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

"Tamati ya droo hii itakuwa ni wiki ya mwisho ya siku ya dabi ambapo tutakuwa na washindi 100 wa Mtoko wa Kibingwa," amesema Maligana na kuongeza.

"Ili kushinda, ni kucheza na Betika, na kuweka mikeka mitano kwa siku yenye dau la Sh 500 kila mkeka ambapo unaingia kwenye droo hiyo moja kwa moja hata kama mkeka wako utachanika.

"Ni rahisi kushinda, Betika Mtoko wa kibingwa, mshirikia anaweza kuweka bashiri zake katika ligi mbalimbali ikiwepo ya EPL, LaLiga, Bundesliga, Serie A na Ligi ya Bongo ikiwamo mechi ya Simba na Yanga, washindi wetu kutoka nje ya Dar es Salaam watasafiri kwa ndege, kabla ya dabi kutakuwa na pati ya mabingwa sanjari uchambuzi wa mechi ya dabi na matukio mengine mbalimbali na Aprili 16 washindi wetu watakwenda uwanjani kwa king'ora kuishuhudia dabi ya watani,".

Afisa Habari wa Betika, Rugambwa Juvenalius alisema droo ya Mtoko wa Kibingwa inahusisha pia wachezaji wa Kitonga Jackpoti na Casino Jackpoti ambao wataingia moja kwa moja bila kujali matokeo ya bashiri zao kwenye mikeka hiyo.