Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mary alia na Sh1.75 milioni ya Geita Queens

MARY Pict

Muktasari:

  • Mbali na changamoto za matibabu, Marry anadai pia kulikuwa na mgogoro kuhusu mkataba wake, akisema alisaini mkataba wa miaka miwili lakini baadaye akaelezwa kuwa mkataba uliowasilishwa ulikuwa wa miezi tisa.

MCHEZAJI wa Geita Gold Queens, Marry Mjema amesema licha ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuamuru klabu hiyo kumlipa mshahara wake wa Sh1.75 milioni, hadi sasa hajapokea fedha hizo licha ya uamuzi huo kutolewa mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza na Mwanaspoti Marry anasema matatizo yake yalianza mwaka 2023 katika mchezo wa robo fainali wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Masala Princess uliopigwa Uwanja wa Nyamagana.

Anadai kuwa dakika ya 86 alipata jeraha la goti baada ya kugongwa kwa nyuma, lakini pamoja na maumivu hayo aliendelea na safari ya timu hadi kufanikisha kupanda Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL).

Anadai baada ya timu kupanda Ligi Kuu na kuanza maandalizi ya msimu wa 2023/24, hakupata matibabu aliyokuwa akiyatarajia, akieleza kuwa alipelekwa kwa waganga wa asili badala ya hospitali.

MAR 01

Marry pia anadai alipokuwa akifuatilia haki zake, aliwahi kupewa kauli zilizomkatisha tamaa, huku akieleza kuwa kipindi hicho kilikuwa kigumu zaidi kutokana na changamoto za kifamilia.

“Mimi ndiyo baba na mama kwenye familia. Niliwaomba mshahara nikamtibie baba yangu aliyekuwa anaumwa sana Moshi, wakakataa. Babangu alifariki nikiwa sina hata senti ya kumsaidia,”  anasimulia Marry kwa uchungu.

Mbali na changamoto za matibabu, Marry anadai pia kulikuwa na mgogoro kuhusu mkataba wake, akisema alisaini mkataba wa miaka miwili lakini baadaye akaelezwa kuwa mkataba uliowasilishwa ulikuwa wa miezi tisa.

Hata hivyo, suala hilo liliwasilishwa katika Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya uamuzi.

MAR 02

Kwa mujibu wa barua rasmi ya TFF yenye kumbukumbu TFF/ADM/DLM .163.2026 ya Mei 10, 2026, kamati hiyo ilisikiliza shauri la Merry dhidi ya Geita Queens kuhusu madai ya mishahara na gharama za matibabu.

Baada ya kupitia maelezo na nyaraka zilizowasilishwa, kamati ilibaini kuwa mchezaji alikuwa hajalipwa mishahara ya miezi saba, huku mkataba wake ukitambuliwa kuwa wa miezi tisa na tayari akiwa amelipwa mishahara ya miezi miwili. TFF iliiamuru Geita Queens kumlipa jumla ya Sh1,750,000 ikiwa ni mishahara yake iliyobaki.

“Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),katika kikao chake cha tarehe 22/04/2026, ilisikiliza shauri la mchezaji Merry Elia Mjema dhidi ya Geita Queens Football Club kuhusu madai ya mishahara sh. 5,500,000 (milioni tano na laki tanu) na gharama za matibabu sh. 48,844,680 (milioni arobaini na nane, laki nane na arobaini na elfu, na mia sita themanini),” ilisema taarifa hiyo ikongeza

“Baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, na kupitia nyaraka zilizowasilishwa, Kamati ilijiridhisha kuwa mchezaji bado anadai mishahara ya miezi saba (7). Mkataba wa mchezaji ulikuwa wa miezi tisa (9), na tayari alikuwa amelipwa mishahara ya miezi miwili (2), hivyo kubaki mishahara ya miezi saba (7),”

MAR 03

“Kila mwezi mchezaji alikuwa analipwa sh. 250,000 (laki mbili na nusu). Hivyo jumla ya mishahara anayodai ni sh. 1,750,000 (milioni moja, laki saba na elfu hamsini).Kwa kuzingatia hayo, Kamati imeiamuru Klabu ya Geita Queens kumlipa Merry Elia Mjema sh. 1,750,000 kama mishahara yake yote iliyobakia na ambayo hajalipwa. Wako katika maendeleo ya mpira wa miguu.”

Hata hivyo, Marry amesema kuwa licha ya uamuzi huo kutolewa tangu Mei mwaka huu, hadi sasa hajapokea fedha hizo.

Anasema hali hiyo imeendelea kuongeza ugumu wa maisha yake wakati ambapo bado anakabiliwa na changamoto za kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji mara tatu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa msaada wa Jeshi.

Marry anasema hawezi kukimbia na mguu wake huvimba kila anapojaribu kufanya kazi nzito. Kutokana na hali hiyo, ndoto zake za kuendelea na soka zimefifia na sasa anatamani kupata mtaji wa biashara ili kuanza maisha mapya nje ya uwanja.

Mwanaspoti ilimtafuta Meneja wa Geita Gold Queens, Sabina Mkama, ili kupata upande wa klabu kuhusu madai hayo. Sabina amesema anafahamu kuwepo kwa suala hilo, lakini hakuwa tayari kutoa maelezo ya moja kwa moja kuhusu hatua zilizofikiwa.

“Yeye Marry anajua sitakuwa na majibu ya moja kwa moja, japokuwa kesi naijua. Anajua nani wa kuwasiliana naye. Mimi alinitafuta sikuwepo, maelekezo yote alipewa. Mimi ni mshikaji wake sana, sijafuatilia waliishiaje,” amesema Sabina.

Mwanaspoti ilifanya jitihada za kumtafuta Ofisa Mtendaji Mkuu wa Geita Gold Queens, Paulo Ojina ili kuzungumzia madai hayo hazikufanikiwa kwani hakupokea simu hadi habari hii inaandikwa. Kadhalika, Mwenyekiti wa Kamati ya Hadhi za Wachezaji wa TFF, Evans Mgeusa, hakupatikana.