Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makalla amtupia kijembe kiaina Manara

Muktasari:

  • Akizungumza na Wanachama waliojitokeza katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, Makalla amesema Simba kumpa nafasi Ahmed Ally imempata mtu sahihi zaidi kuliko aliyeondoka.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ambaye ni mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa Uchaguzi wa Simba unaofanyika leo Januari 29,  amemtupia kijembe aliyekuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara.

Akizungumza na Wanachama waliojitokeza katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, Makalla amesema Simba kumpa nafasi Ahmed Ally imempata mtu sahihi zaidi kuliko aliyeondoka.

"Wanasimba mnapaswa kujivunia sana kwa kupata mtu sahihi kama, Ahmed Ally kwani ameonyesha ana uwezo mkubwa wa utambuzi wa mambo," amesema Makala akishangiliwa kwa nguvu na maelfu ya Wanachama waliojitokeza kwenye Ukumbi huo.

Manara aliyejizoelea umaarufu kabla ya kujiunga na Yanga alikuwa msemaji wa Simba.