Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabula aanza na mguu mzuri Algeria

MABULA Pict

Muktasari:

  • Mabula, ambaye kwenye mchezo huo alianzia benchi alieleza kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa na timu yake ilifanikiwa kupata pointi tatu muhimu.

KIUNGO wa Mtanzania, Alphonce Mabula ameanza na mguu mzuri kwenye Ligi Kuu ya Algeria baada ya chama lake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MB Rouissat katika mchezo wao wa kwanza.


Mabula, ambaye kwenye mchezo huo alianzia benchi alieleza kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa na timu yake ilifanikiwa kupata pointi tatu muhimu.

Akizungumza na Mwanaspoti Mabula amesema “Mechi ilikuwa nzuri yenye ushindani. Tumefanikiwa kushinda mchezo wetu wa kwanza na kuanza msimu vizuri, hilo ndilo jambo la msingi,”

Akizungumzia mazingira ya ligi hiyo, Mabula amesema amevutiwa na kiwango cha ushindani huku akidai Ligi ya Algeria ina ushindani unaoweza kufananishwa na baadhi ya ligi za Ulaya, jambo ambalo limeifanya safari yake mpya kuwa yenye changamoto na kuvutia.

“Mazingira ni mazuri uwanjani. Kwa ambao hawaijui Ligi ya Algeria, ni levo kama ligi za Ulaya kabisa kitu kizuri kinachonifurahisha ni kwamba kila timu ina mashabiki, kwa hiyo viwanja vyote kujaa ni jambo la kawaida kwao,” amesema.

Mabula amesema hali hiyo inaonyesha wazi ukubwa wa ushindani wa ligi hiyo, akisisitiza kuwa si mashindano yanayotawaliwa na klabu mbili au tatu pekee, bali timu nyingi zina uwezo wa kufanya vizuri na kupambana kwa ajili ya mataji.

Alitolea mfano wa USM Alger ambao walifanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika, lakini msimu uliopita wakamaliza katika nafasi ya 11 kwenye ligi, akisema hilo ni ushahidi wa namna ushindani ulivyo mkubwa na matokeo yanaweza kubadilika kutoka msimu mmoja hadi mwingine.

“Ni ligi ambayo ina timu 12 zote ni kubwa hapa Algeria. Unaweza kuona hata USM Alger walichukua kombe, lakini ukiangalia msimamo wa msimu ulioisha wamemaliza nafasi ya 11. Hapo inajieleza kabisa ni aina gani ya ligi,” amesema Mabula.

Mabula ambaye alitambulishwa hivi karibuni kwenye kikosi cha JS Kabylie ya Algeria akitokea Shamakhi FC ya Ligi Kuu Azerbaijan alipokuwa na msimu bora.