Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mabula atua JS Kabylie akiwatosa Waturuki

MABULA Pict

Muktasari:

  • Mabula ametua JS Kabylie akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Shamakhi ya Azerbaijan.

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Alphonce Mabula, amejiunga na JS Kabylie ya Algeria leo Jumatatu, Agosti 31, 2026.

Mabula ametua JS Kabylie akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na Shamakhi ya Azerbaijan.

“Hatua mpya inaanza. Karibu Alphonce Msanga ndani ya JS Kabylie,” imeandika JS Kabylie katika utambulisho wake wa Mabula.

Mabula anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji, alikuwa mchezaji tegemeo wa Shamakhi msimu uliopita ambapo aliichezea idadi ga mechi 28 za Ligi Kuu ya Azerbaijan.

Katika mechi hizo 28, Mabula alifunga mabao mawili huku akionyeshwa kadi tisa za njano.

MABU 01

Pia ni mchezaji tegemeo wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ aliyoichezea mechi 10 huku nne zikiwa ni za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Usajili wa JS Kabylie kwa Mabula unazika taarifa za kiungo huyo kwenda Uturuki kujiunga na Kasimpasa ambayo inatajwa kwamba ilikuwa inamuwania.