Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dili la Mabula Yanga lilivyokwama

MABULA Pict


BAADA ya dili la kwenda Yanga kukwama, inaelezwa kiungo wa Taifa Stars, Alphonce Mabula, yuko kwenye hatua nzuri ya kutimkia Ulaya baada ya mazungumzo na Kasimpasa ya Uturuki kufikia hatua nzuri.


Mabula, ambaye amemaliza mkataba wake na Shamakhi FC ya Azerbaijan Juni 30, 2026, amekuwa akihusishwa na klabu mbalimbali tangu aonyeshe kiwango kizuri akiwa katika Ligi Kuu ya Azerbaijan.


Mwanaspoti liliripoti Aprili 2026 kwamba Kasımpasa ilikuwa ikifuatilia kwa karibu uwezekano wa kumsajili kiungo huyo, huku mazungumzo ya awali yakifanyika kati ya klabu hiyo ya Uturuki na uongozi wa mchezaji.

Baadaye, Yanga iliingilia dili hilo ikisaka saini ya kiungo huyo, huku taarifa zikieleza kwamba ofa ya Kasımpaşa ilikuwa imefikia Sh2 bilioni.

MABU 02

Yanga ilijaribu kumrudisha nyumbani kiungo huyo ambaye amekuwa akicheza soka la kulipwa Ulaya kwa takribani miaka minne, lakini dili hilo likakwama baada ya pande hizo kushindwa kufikia makubaliano ya kifedha.


DILI LA YANGA LILIVYOKUWA

Yanga ilianza mazungumzo na Mabula ikiwa na nia ya kuongeza nguvu katika eneo la kiungo mkabaji kwa msimu huu wa 2026-2027.

Mabula alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa wakiwavutia mabosi wa Yanga kutokana na uzoefu wake wa kucheza soka Ulaya, huku pia akiwa bado kijana mwenye nafasi ya kuendelea kukua akiwa na miaka 23.

MABU 01

Mwanaspoti liliripoti Julai 2026 kwamba Yanga ilikuwa tayari imeanza mazungumzo na Mabula na ilikuwa imempa ofa nzuri, huku mchezaji huyo akirudi hapa nchini kwa mapumziko baada ya kumaliza mkataba wake na Shamakhi.

Hata hivyo, chanzo kinaeleza kuwa upande wa Mabula ulikuwa ukiangalia ofa yenye thamani ya takribani Sh1.5 bilioni kwa ajili ya uhamisho wake kwenda Yanga, huku pia ukihitaji mshahara wa karibu Dola 14,000 kwa mwezi, kiasi kinachokadiriwa kuwa zaidi ya Sh37 milioni za Tanzania.

Lakini Yanga ilifikia zaidi ya Sh600 milioni kwenye uhamisho wake, lakini inaelezwa kiasi hicho hakikukidhi mahitaji ya upande wa mchezaji na kwamba viongozi wa Wananchi hawakumrudia tena.

MABU 01

KUIBUKIA KASIMPAŞA

Kasımpaşa imekuwa ikimfuatilia Mabula kwa muda mrefu tangu miezi sita nyuma wakati akibakiza miezi sita ndani ya Shamakhi FC.

Taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata ni kwamba, klabu hiyo ilikuwa imevutiwa na uwezo wa Mabula katika eneo la kiungo, hasa uwezo wake wa kukaba, nidhamu ya mchezo na kuanzisha mashambulizi.

Kwa sasa, mazungumzo kati ya Kasımpaşa na uongozi wa Mabula yanaendelea vizuri, huku klabu hiyo ikiwa karibu kufikia kiwango cha fedha kinachotakiwa na upande wa mchezaji.

Inaelezwa awali uongozi wa Mabula ulikuwa ukiangalia kiasi cha karibu Sh2.5 bilioni, huku Kasımpaşa ikiwa kwenye hatua za mwisho za kusogea karibu na kiwango hicho.

MABU 03

"Ni kweli kuna ofa nyingi ambazo bado tunazijadili, kuna timu kutoka Azerbaijan lakini ya Uturuki iko karibu zaidi na siriazi kama mambo yatakuwa sawa atajiunga nayo," amesema mmoja wa watu wa karibu wa mchezaji huyo.

Jambo lingine linaloipa Kasımpaşa nafasi kubwa ya kumsajili Mabula ni kwamba, klabu hiyo ilikuwa tayari imeanza mazungumzo na kiungo huyo kabla hata hajaondoka Shamakhi. Hata mchezaji mwenyewe msimamo wake wa kwanza ni kucheza ligi kubwa Ulaya na inaonekana Uturuki ni sehemu anayoweza kuendana nayo.

Kwa upande wa Mabula, uamuzi wake unaonekana kuangalia zaidi mambo matatu; fedha, nafasi ya kucheza na mazingira yatakayomuwezesha kuendelea kupiga hatua katika soka la Ulaya.

Kwenye moja ya mahojiano aliyowahi kufanya na Mwanaspoti, alisema: "Kila mchezaji ana malengo yake lakini kwangu bado kijana na moja ya tamanio langu ni kuendelea kucheza Ulaya na kwenye ligi kubwa ili nipate uzoefu na kuisaidia timu yangu ya taifa."

MABU 02

AKIJIUNGA KASIMPAŞA

Iwapo atakamilisha dili hilo, Mabula atakuwa Mtanzania mwingine kucheza Ligi Kuu ya Uturuki, akifuata nyayo za Novatus Miroshi anayekipiga Göztepe na Mbwana Samatta aliyeitumikia Fenerbahce kuanzia 2020 hadi 2023.

Mabula atakuwa anajiunga na ligi yenye mastaa mbalimbali wa soka dunia. Miongoni mwao ni nyota za zamani wa Liverpol, Mohamed Salah ambaye ametambulishwa Trabzonspor.

Kama pande zote mbili zitafikia makubaliano, huenda Mtanzania huyo akawa mmoja wa wachezaji wapya wa Tanzania kuendelea kuiwakilisha nchi katika ligi kubwa barani Ulaya.

MABU 01

Mabula alianza safari yake ya soka la kulipwa Ulaya mwaka 2022 baada ya kuondoka Alliance FC ya Mwanza na kutua Spartak Subotica ya Serbia pia kuitumikia RFK Novi Sad, kisha Shamakhi FC ya Azerbaijan msimu wa 2024-2025.

Akiwa Shamakhi, alikuwa mchezaji muhimu kikosini hapo na msimu wa mwisho alicheza mechi 25 akifunga mabao mawili.

Kiwango hicho ndicho kilichomfanya aanze kuangaliwa na klabu mbalimbali, huku Kasımpaşa ikiwa miongoni mwa zinazotaka kumsogeza hatua nyingine kwenye maisha yake ya soka.