Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ligi ya ng'ombe Dar kutoa elimu ya uzazi na mpango

Shirika lisilo la Kiserikali la CAFLO limeanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wenye miaka 14 hadi 25 waliopo katika kata tano za jiji la Dar es Salaam kwa lengo la kuwapatia elimu na mbinu za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Mashindano hayo waliyoyaita ligi ya ng’ombe yanatekelezwa na shirika hilo chini ya ufadhili wa GGML Kilimanjaro Challenge Against HIV/AIDS Trust, Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) na Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam yanalenga pia kutoa elimu kwa vijana hao kuhusiana na masuala ya uzazi wa mpango.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Msaidizi wa Kudhibiti Ukimwi Halmashauri ya jiji, Anselimina Mfinanga alisema anatambua kuwa michezo ni afya hivyo amewataka vijana waliopata nafasi ya kushiriki kuhakikisha wanacheza kwa amani na kupata elimu hiyo.

Alisema uwepo wa ligi hiyo katika kata hizo tano ambazo ni Vingunguti, Tabata, Mnyamani, Kipawa na Buguruni itatoa fursa kwa vijana wengi kupata mbinu mpya ya kujikinga na maambukizi ya VVU na kuimarisha afya zao.

Naye Mratibu wa Miradi kutoka CAFLO, Emmanuel Ngazi alisema jumla ya timu 16 za vijana wa kiume kutoka katika kata hizo tano zitashiriki huku mshindi wa kwanZatapatiwa zawadi ya ng’ombe mwenye thamani ya Sh. Milioni 1.5.

Alisema matarajio kutoka kwenye mashindano hayo ni kuwahamasisha vijana kutumia michezo kama njia mojawapo ya kujikinga na maambukizi ya VVU na kujituma kufanya kazi kwa bidi kwa ajili ya kujiletea maendeleo endelevu.

“Wadau mbalimbali tunaomba waendelee kujitokeza kuwajengea uwezo vijana hawa juu ya kujikinga na maambukizi ya VVU, mashindano haya yatawafanya vijana hawa kuendelea kuwa na afya njema na watashiriki kikamlifu katika shughuli za kimaendeleo,” alisena Ngazi.

Hata hivyo Ngazi alisema wataandaa pia mashindano ya mpira wa pete kwa vijana wa kike kwa ajili ya kuwaelimisha na kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.

“Utaona mradi huu umewalenga zaidi vijana wenye umri mdogo kuanzia miaka 14 hadi 25 kutokana na kwamba kundi hili lipo katika hatari kubwa la kupata maambukizi,” alisema

Mashindano hayo yameanza kutimua vumbi rasmi Mei 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa Sinai uliopo mtaa wa Faru kata ya Mnyamani kwa timu ya Msimamo kutoka Kata ya Mnyamani  kuwafunga timu ya Karakata kutoa kata ya Kipawa bao 3 kwa bila.