KVZ watuma salamu kwa Wasudan

Friday November 27 2020
KVZ PIC
By Mwandishi Wetu

WAWAKILISHI kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, KVZ kutoka kisiwani Unguja leo Ijumaa watacheza mechi yao ya awali kwenye michuano hiyo dhidi ya AL Atbara ya Sudan huku wakitamba ushindi ni lazima.

KVZ itakuwa ugenini ambapo mechi yao itachezwa kuanzia saa 9:00 alasiri leo wakati Namungo kutoka Bara na wao watacheza mechi hiyo leo dhidi ya Al Rabita, mechi itachezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Sudan, Nahodha wa KVZ, Suleiman Abdi ameiambia Mwanaspoti Online leo Ijumaa Novemba 27, 2020 kuwa kila kitu kwako kipo vizuri wanachosubiri ni kukabiriana na wapinzani wao.

"Tuliwafuatilia wapinzani wetu kwa njia ya mtandao lakini hatukutaka kuiamini sana mitandano maana wakati mwingine video za mitandaoni hazionyeshi kila kitu.

"Hivyo tulijipanga kwa maandalizi yetu kuwa tunakuja huku kupambana kupata ushindi, ingawa kucheza ugenini ni kugumu lakini lazima tuonyeshe nia yetu ya kushinda na tunaamini matokeo yatakuwa mazuri.

"Hakuna anayeingia uwanjani akitaka matokeo mabaya, kila mmoja anataka ushindi hivyo ikitokea matokeo yakawa tofauti basi itakuwa ni moja ya matokeo ya soka ambayo yatatufanya tujipange zaidi kwenye mechi ya marudiano tutakayokuwa nyumbani," amesema Abdi.

Advertisement
Advertisement