Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kuna vita usiyoijua Championship

Muktasari:

  • Juzi, Pamba ilikwea katika nafasi ya pili baada ya kuifumua Cosmopolitan kwa mabao 2-1 ugenini jijini Dar es Salaam, na kuchupa kutoka nafasi ya nne ikiishusha Mbeya Kwanza na TMA FC katika msimamo unaongozwa na KenGold yenye pointi 36 katika mechi 16 ilizocheza.

Siku moja baada ya Pamba kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Championship ikiwa na alama 34, imebainika vita nyingine mpya katika mashindano hayo ikihusisha hesabu nzito za timu zote 16 zinazopambana kuwania kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao. 

Juzi, Pamba ilikwea katika nafasi ya pili baada ya kuifumua Cosmopolitan kwa mabao 2-1 ugenini jijini Dar es Salaam, na kuchupa kutoka nafasi ya nne ikiishusha Mbeya Kwanza na TMA FC katika msimamo unaongozwa na KenGold yenye pointi 36 katika mechi 16 ilizocheza.

Hata hivyo, ushindi wa Pamba kumbe unaibeba kutokana na namba tu za pointi, lakini timu hiyo iliyoshinda michezo 10 inalingana na Biashara United pamoja Mbeya Kwanza ambazo pia zimeshinda idadi hiyo ya michezo, zikiifuata KenGold iliyoshinda mechi 11. 

Timu zingine zilizokamata nafasi za juu kwa mechi nyingi zilizoshinda ni TMA FC iliyoshinda tisa ikishoka namba nne katika msimamo ikiwa na alama 33, huku Mbuni FC ikishinda mechi nane ilhali katika msimamo ikishika nama sita na pointi 27.

Ukiachana na timu hizo, Mbeya City na Polisi Tanzania zimeshinda mara sabaa zikiwa nafasi ya saba na nane mtawalia, huku Stand United ikishika nafasi ya tisa kwa ushindi wa michezo sita, ikifuatiwa na Green Warriors, FGA Talents na Pan Africans zilizoshinda michezo minne zikifuatana kwa mtiririko huo katika msimamo.

Transit Camp na Cosmopolitan zimeshinda mechi tatu zikishika namba 13 na 14, huku Copco ikishinda mechi tatu ikiwa ya 15 katika msimamo unaofungwa na Ruvu Shooting ambayo haina ushindi wowote.

Hata hivyo, maajabu mengine katika msimamo huo yapo katika timu iliyo na sare nyingi ambayo ni TMA FC iliyosare mara sita sawa na Green Warriors, huku Cosmopolitan na Transit Camp zikiifuata kwa sare tano ilhali Pamba, Mbeya City na Stand United zina sare nne.

Timu zenye sare tatu ni Copco, Pan Africans, FGA Talents, Mbuni na Biashara United huku Mbeya City, Polisi Tanzania na Ruvu Shooting zikiwa zimetoka sare mara mbili katika michezo 16.

Kati ya timu 16 zinazowania kupanda Ligi Kuu msimu ujao zile mbili zilizo mkiani yaani Ruvu Shooting na Copco zimechapwa jumla ya mechi 24 zilizocheza ikiwa ni vipigo viwili zaidi ya vile ambavyo timu saba kwa ujumla wake zilizo juu mwa msimamo zimevipata. Timu hizo kuanzia namba moja hadi saba zimepoteza michezo 22 kwa ujumla wake.

Upande wa mabao ya kufunga, safu ya ushambuliaji ya KenGold imeendelea kuwa bora zaidi ikifunga mabao 29, ikifuatiwa na Biashara United iliyotupia 28, huku Pamba ikiwa ya tatu na mabao 24 inayofuatiwa na Mbeya Kwanza na Mbuni zilizofunga mabao 23 kila moja. Timu zingine 12 zimefunga chini ya mabao 20. Kwa ujumla timu zote zimefunga mabao 286 zikiwa na jumla ya pointi 355.