Kocha Simba kutajwa
Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umesema wiki hii utamtangaza rasmi mrithi wa Sven Vandenbroek pamoja na kocha wa makipa atakayechukua nafasi ya Muharami Mohamed.
Simba inafanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi ingawa kocha msaidizi, Seleman Matola atabaki nafasi hiyo.
Makocha watatu wanatajwa kuwania nafasi ya Sven ambao ni Clinton Larsen, Adel Amrouche na Eric Tinkle, huku Idd Salim raia wa Kenya akitajwa kuja kuwa kocha wa makipa, nafasi iliyokuwa wazi mapema kabla ya kutimka kwa Sven.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema mchakato unaendelea vizuri na umechukuwa muda kidogo kukamilika kwani walihitaji umakini zaidi kufanya uamuzi na sasa ni kumtangaza tu.