Kocha Sheha aahidi makubwa Uhamiaji
KOCHA MKUU wa timu ya Uhamiaji, Sheha Khamis amepanga kufanyakazi kwa umakini ili kusimamia malengo mapya ya msimu wa 2026-2027.
Amesema, anatumia uzoefu wake kuijenga timu hiyo kuwa na ushindani kwa kuleta ladha tofauti kwenye Ligi Kuu ya Zanzibar msimu mpya unaotarajiwa kuanza hivyo karibuni.
Kocha Sheha amesema, kwa sababu viongozi hao wameamua kumuamini kwa kumkabidhi kikosi cha timu hiyo anaahidi kutowaangusha. “Kwasasa kikosi kinajifunza mbinu za kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zao kwa kujijenga kwa pamoja na ushirikiano,” amesema
Kocha huyo amesema, anachohitaji kutoka kwa wachezaji hao ni ushirikiano na umakini wao kwa lengo la kuitengeneza Uhamiaji anayoitaka.
Amesema, Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu inakabiliwa na mambo mengi hivyo kuna ugumu ndani yake ambao unazilamisha timu kutumia muda vizuri kujiandaa.
Hatahivyo, amesema mpira umekuwa biashara na ajira kwa mantiki hiyo kila mmoja atakuwa tayari kuonesha uwezo wake.
Hivyo, amewasihi wachezaji wa timu hiyo kutokukubali kuachwa nyuma na wengine ni wakati wa kupambania malengo ya timu.