Sheha amrithi AbdulSaleh Uhamiaji
Muktasari:
- Uhamiaji ilimaliza msimu wa 2025-2026 ikiwa nafasi ya tano na pointi 51, huku KVZ ikiwa bingwa wa ligi hiyo kwa alama 67 tofauti ya alama tatu na JKU iliyomaliza ya pili.
BAADA ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa Uhamiaji, AbdulSaleh Mohamed kujiunga na JKU, timu hiyo imepata mrithi wa kuinoa msimu ujao wa 2026-2027.
Katika taarifa iliyotolewa na Uhamiaji, imemtangaza rasmi Sheha Khamis kuwa kocha wao mkuu.
"Tunapenda kuwatangazia rasmi kuwa Kocha Sheha Khamis ni kocha wetu Mkuu kuanzia sasa, karibu kwenye familia yetu, kocha wa viwango vya juu," ilisema taarifa hiyo.
Msimu wa 2025-2026, kocha huyo aliinoa Muembe Makumbi iliyomaliza Ligi Kuu Zanzibar nafasi ya 10 ikikusanya pointi 42 kati ya mechi 30 ilizocheza.
Uhamiaji ilimaliza msimu wa 2025-2026 ikiwa nafasi ya tano na pointi 51, huku KVZ ikiwa bingwa wa ligi hiyo kwa alama 67 tofauti ya alama tatu na JKU iliyomaliza ya pili.