Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uhamiaji FC kujipanga kwa msimu mpya

Muktasari:

  • Timu hiyo katika kuboresha kikosi, tayari imetangaza kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kumteua Sheha Khamis aliyechukua nafasi ya Abdulsaleh Muhammed.

UHAMIAJI FC, ina mikakati ya kuhakikisha katika msimu wa 2026-2027, inafanya vizuri zaidi ya ilivyokuwa 2025-2026 na ilimaliza nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar ikikusanya pointi 51.

Timu hiyo katika kuboresha kikosi, tayari imetangaza kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi kwa kumteua Sheha Khamis aliyechukua nafasi ya Abdulsaleh Muhammed.

Katika hatua nyingine, Uhamiaji imeachana na wachezaji saba ambao ni Moh’d Mussa, Adil Sultan, Yussuf Kahata, Yussuf Abdu, Kassim Suleiman, Kessy Bakar Kessy na Salum Abdulla Salum.

Pia timu hiyo imewatambulisha kiungo Masoud Ali Moh’d ‘Kichuda’ akitokea Chipukizi, mshambuliaji Ajib Mohamed kutoka Malindi, kiungo Ikram Said na mabeki wa kati waliotokea Shalke FA ambao ni Abdillah Mussa na Seif Nassor.

Ofisa Habari wa Uhamiaji, Mwinyi Ali Hamad, alisema: “Tumeacha wachezaji wa kutosha kwa sababu tunataka kukisuka upya kikosi chetu katika sura mpya zenye uwezo.

“Nafasi ambazo tunaziboresha zaidi ni ulinzi pamoja na ushambuliaji ili katika msimu ujao Uhamiaji tuione katika levo nyingine kubwa ambayo tunaamini tunakwenda kimataifa.”