Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Polisi Zanzibar afichua jambo

KOCHA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo iliyopigwa Agosti 29, 2026 kwenye Uwanja wa Mao B kisiwani Unguja, Polisi iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Rashid Messi dakika ya 74.

POLISI Zanzibar inayoshiriki Ligi Kuu, imetaja siri ya ushindi wao dhidi ya KVZ ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo.

Katika mechi hiyo iliyopigwa Agosti 29, 2026 kwenye Uwanja wa Mao B kisiwani Unguja, Polisi iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Rashid Messi dakika ya 74.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Msaidizi wa Polisi Zanzibar, Awesu Maulid Suleiman amesema vipaji vipya vilivyoandaliwa na timu ndio sababu ya kupata ushindi huo.

Amesema timu hiyo ina wachezaji wengi wapya na wanatumia nguvu kubwa kuiunganisha timu ndiyo maana imepata matokeo hayo kwenye mechi yake ya kwanza.

"KVZ tuliwashinda zaidi eneo la kati kwa sababu wachezaji wao ni watu wazima, wa kwetu wadogo, hivyo wakashindwa kuhimili mikiki," amesema.

Kocha huyo amesema wachezaji wa KVZ waliingia uwanjani wakiwa na matokeo yao mkononi jambo ambalo liliwafanya kujiamini zaidi na hatimaye kupoteza.

"Kama wataendelea kujiamini kwa sababu walitwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita, basi watateseka sana na wanachopaswa kutambua uamuzi wa mpira humalizika dakika 90 uwanjani na sio mdomoni," amesema kocha huyo huku akisisitiza katika mpira wa miguu hutakiwi kumdharau yeyote.

Kocha huyo, amewataka mashabiki wa Polisi Zanzibar kuendelea kushikana kwa vipindi vyote vya furaha na huzuni huku lengo likiwa ni kufanya vizuri.