Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha JKU afichua siri ya kupambana hadi mwisho

JKU Pict

Muktasari:

  • Hadi dakika ya 70, Mlandege ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, lakini JKU ikasawazisha dakika ya 73 na 80, kisha ikaongeza lingine dakika 80, kabla ya Mlandege kukomboa dakika ya 89 na kufanya mechi kumalizika kwa sare.

Kocha Mkuu wa JKU, Abdul-Saleh Mohammed, amesema kurejesha mabao mawili ndani ya muda mfupi si jambo la kushangaza bali ni matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya katika uwanja wa mazoezi.

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya kukiongoza kikosi chake kutoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mlandege katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliochezwa Agosti 30, 2026.

Hadi dakika ya 70, Mlandege ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-0, lakini JKU ikasawazisha dakika ya 73 na 80, kisha ikaongeza lingine dakika 80, kabla ya Mlandege kukomboa dakika ya 89 na kufanya mechi kumalizika kwa sare.

Amesema hiyo ndio miongoni mwa mbinu walizokuwa wakifanyiakazi uwanja wa mazoezi namna ya kupambana hadi dakika ya mwisho bila kukata tamaa hata wanapokuwa nyuma kwa mabao.

JK 01

Kocha huyo amesema baada ya kufungwa mabao hayo mawili na Mlandege, wachezaji hawakupoteza mwelekeo wala kuingiwa na hofu, badala yake waliendelea kuamini katika uwezo wao wa kubadilisha matokeo.

"Mazoezini tumekuwa tukisisitiza umuhimu wa kuwa na umakini, uvumilivu na nidhamu ya kiuchezaji katika kila hatua ya mchezo na tunawafundisha wachezaji kuamini kwamba matokeo yanaweza kubadilika muda wowote," amesema.

Amesema, wachezaji wamekuwa wakipewa maelekezo ya namna ya kuongeza kasi ya mashambulizi, kutumia nafasi na kubaki na utulivu wanapokuwa katika presha.

JK 02

Kwa upande mwingine, kocha huyo aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha moyo wa kupambana na kutokubali kushindwa mapema.

Mwisho kabisa, alibainisha kwamba, matokeo hayo ni faraja kwa timu lakini bado kuna maeneo ambayo wanahitaji kuyafanyia kazi ili kuwa bora zaidi katika michezo ijayo.

JKU inatarajiwa kushuka tena dimbani Septemba 17, 2026 kucheza mechi ya pili ya Ligi Kuu Zanzibar dhidi ya KVZ kwenye Uwanja wa Mao A, Unguja.