Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha AbdulSaleh abeba matumaini JKU

JKU pict

Muktasari:

  • Timu hiyo inaendelea kusuka kikosi chake cha msimu mpya baada msimu wa 2025-2026 kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar kwa tofauti ya alama tatu na KVZ iliyotwaa ubingwa.

BAADA ya JKU kumpa Kocha AbdulSaleh Abdallah majukumu ya kuinoa timu hiyo, uongozi wa klabu hiyo umesema una matumaini ataifikisha kwenye malengo yaliyopo msimu ujao 2026-2027.

Kocha huyo ambaye amesaini mkataba wa mwaka kikosini hapo, amechukua mikoba ya Ali Bakari aliyeiongoza JKU msimu uliopita.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa JKU, Shadhil Khatib Shadhil amesema kocha huyo ataongeza nguvu katika benchi la ufundi msimu wa 2026-2027.

Amesema uongozi umevutiwa na kocha huyo kwa uzoefu wake na namna anavyoifanya timu kuwa na ushindani, jambo lililowafanya kuona ni chaguo sahihi upande wao.

“Uongozi utashirikiana naye na kuhakikisha tunampa mazingira mazuri ya kufanyia kazi pamoja na usajili utakaokidhi mahitaji ya timu,” amesema kiongozi huyo.

Pia, amesema matarajio ya timu hiyo ni kuona inarejea katika ushindani wa juu Ligi Kuu Zanzibar huku kocha huyo akianza majukumu yake rasmi tangu Julai 27, 2026.

Shadhil amesema, endapo kocha huyo atafanya vizuri kwa kuwapa wanachokitarajia, uongozi una mpango wa kumuongezea muda.

Timu hiyo inaendelea kusuka kikosi chake cha msimu mpya baada msimu wa 2025-2026 kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar kwa tofauti ya alama tatu na KVZ iliyotwaa ubingwa.