Mlandege yahitaji kurejesha ubingwa ZPL
Muktasari:
- Mlandege msimu uliopita ilipoteza taji lao kwa KVZ baada ya kushindwa kulitetea na msimu huu wana kazi ya kufanya kuhakikisha wanalirudisha mikononi mwao.
KOCHA Mkuu wa Mlandege, Hassan Ramadha 'Pele' amesema lengo kubwa la timu hiyo msimu wa 2026-2027, ni kurudisha kombe la Ligi Kuu mikononi mwao.
Mlandege msimu uliopita ilipoteza taji lao kwa KVZ baada ya kushindwa kulitetea na msimu huu wana kazi ya kufanya kuhakikisha wanalirudisha mikononi mwao.
Kocha Pele amesema wameshatambua sababu zilizowakwamisha kutetea ubingwa wao kwa hiyo msimu huu hawapo tayari kurudia makosa waliyofanya msimu uliopita.
Pele amesema kwa mtazamo wake msimu ujao unaweza kuwa mgumu kuliko uliopita ndiyo maana anataka kuitengeneza timu kuwa imara ambayo itaweza kucheza katika mazingira yoyote.
"Katika dirisha hili kubwa tumetoa wachezaji muhimu lakini Mlandege huwa hatutegemei mchezaji mmoja, hivyo tunajipanga kuziba mapengo kwenye nafasi zilizowachwa wazi," amesema
Kocha huyo, amesema mechi tano za mwanzo ni ngumu lakini watapamba kuhakikisha wanafanya vizuri kwa sababu ndizo zinazotoa picha ya uelekeo wao.
Mechi hizo ni dhidi ya JKU SC, Polisi SC , KVZ FC, Muembe Makumbi City na Chipukizi United.