Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Yanga atimkia Mashujaa

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo kabla ya kujiunga na Mashujaa msimu huu, amezitumikia timu zote nne zenye ushindani wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, akipitia JKT Queens, Simba Queens na Yanga Princess na kujenga jina kama mmoja wa viungo bora nchini.

ALIYEKUWA kiungo wa Yanga Princess, Maimuna Hamis ‘Mynaco’ amejiunga na Mashujaa Queens kwa mkataba wa mwaka mmoja kama mchezaji huru.

Nyota huyo kabla ya kujiunga na Mashujaa msimu huu, amezitumikia timu zote nne zenye ushindani wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, akipitia JKT Queens, Simba Queens na Yanga Princess na kujenga jina kama mmoja wa viungo bora nchini.

Kiongozi mmoja wa Mashujaa Queens, ambaye jina lake tunalo, amesema timu hiyo imefanya usajili mchanganyiko wa nyota wachanga na wenye uzoefu ili kuleta balansi kwenye kikosi kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake.

KIU 01

Amesema baadhi ya wachezaji walioachwa na timu kubwa wana uzoefu wa kutosha wa kushindana kwenye kiwango cha juu, hivyo usajili wao unaaminiwa kuongeza ush indani ndani ya kikosi na kuwasaidia wachezaji vijana kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwao.

“Tumefanya usajili ambao una mchanganyiko wa wachezaji vijana na wenye uzoefu. Kuna baadhi ya wachezaji walioachwa na timu kubwa ambao wana uzoefu wa kucheza mechi kubwa, hivyo tunaamini watatusaidia kuleta balansi kwenye timu,”  amesema kiongozi huyo.

Maimuna, ambaye ni kiungo mwenye uwezo wa kucheza kwa utulivu na kutuliza mchezo eneo la kati, anaingia Mashujaa akiwa na uzoefu wa kutosha wa ligi hiyo, jambo linalotarajiwa kuwa moja ya silaha za timu hiyo msimu ujao.

KIU 02

Kiungo huyo pia amewahi kucheza nje ya Tanzania, akitumikia Zed FC ya Misri kwa misimu miwili kabla ya kurejea nchini .Kipindi hicho kilimpa uzoefu mwingine wa kucheza nje ya mazingira ya soka la Tanzania.

Mynaco pia anaingia Mashujaa akiwa na historia ya mafanikio katika ligi ya ndani, akiwa amebeba mataji matano ya Ligi Kuu ya Wanawake katika vipindi alivyokuwa akizitumikia JKT Queens na Simba Queens. Rekodi hiyo inamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wenye uzoefu wa kushinda mataji katika kikosi hicho kipya.