Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Mtanzania akataa ofa ya Misri aichagua Stars

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Kinda huyo mwenye miaka 19 alijiunga na ENPPI msimu uliopita akitokea Fountain Gate ambako alikuwa kwa mkopo akitokea Azam FC. Konde Boy, ambaye alitokea Azam FC kabla ya kujiunga na ENPPI, amekuwa akifuatiliwa baada ya kuonyesha uwezo wake akiwa katika ligi hiyo.

KIUNGO wa ENPPI ya Ligi Kuu Misri, Mtanzania Arafat Masoud ‘Konde Boy’, amesema ni kweli alitafutwa na viongozi wa soka nchini humo lakini msimamo wake ni kuitumikia timu ya taifa ‘Taifa Stars’.

Kinda huyo mwenye miaka 19 alijiunga na ENPPI msimu uliopita akitokea Fountain Gate ambako alikuwa kwa mkopo akitokea Azam FC. Konde Boy, ambaye alitokea Azam FC kabla ya kujiunga na ENPPI, amekuwa akifuatiliwa baada ya kuonyesha uwezo wake akiwa katika ligi hiyo.

Konde Boy amesema viongozi wa Shirikisho la Soka la Misri walizungumza naye na kumweleza kuhusu uwezekano wa kujiunga na timu hiyo, lakini msimamo wake ni kutaka kuipigania Tanzania.

“Ndiyo, kulikuwa na mazungumzo kuhusu hilo. Viongozi wa Shirikisho walikuwepo, wakaniita na kuniuliza kama nishawahi kuitumikia timu yoyote ya Taifa. Baadaye meneja wangu akaniambia wanataka kuangalia uwezekano wa mimi kucheza U-20, kama itawezekana, ila ni mchakato kidogo,”  amesema.

Hata hivyo, badala ya kuendelea kusubiri mchakato huo, Konde Boy amesema malengo yake yalikuwa wazi tangu alipokuwa akiitumikia Azam FC kucheza soka nje ya Tanzania ili siku moja apate nafasi ya kuitumikia nchi yake.

“Kipindi nipo Azam nilisema ndoto zangu ni kucheza nje kwa ajili ya manufaa ya timu ya Taifa. Sasa nimefika huku, nimepambana na nimepata nafasi ya kuonekana, lakini bado nataka nchi yangu iniamini,” 

“Wakati Misri wanazungumza na mimi ndipo TFF lilituma barua ya kunihitaji katika majukumu ya timu ya Taifa. Kwa jitihada nilizonazo nitapambana ili iwe mwendelezo kwangu, kwa sababu si rahisi kuaminika.