Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichokwamisha dili la Mtanzania Misri

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo aliyeifungia KMC FC bao moja la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, alifikia makubaliano ya kujiunga na Petrojet SC iliyomtumia mkataba, licha ya Klabu ya Petrol Asyout kutoka Misri pia kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

LICHA ya mshambuliaji Mtanzania, Jammy Simba kwenda Misri kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Petrojet SC, lakini dili la nyota huyo limeshindwa kukamilika, baada ya kile kinachodaiwa kukiukwa kwa makubaliano ya mkataba uliokuwepo mwanzo.

Mshambuliaji huyo aliyeifungia KMC FC bao moja la Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026, alifikia makubaliano ya kujiunga na Petrojet SC iliyomtumia mkataba, licha ya Klabu ya Petrol Asyout kutoka Misri pia kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Akizungumza na Mwanaspoti, Simba alisema alifikia uamuzi wa kujiunga na Petrojet SC ingawa dili hilo lilishindwa kufanikiwa, baada ya uongozi huo kwenda kinyume na makubaliano yao ya kimkataba waliyokubaliana kabla ya kwenda Misri.

“Mkataba walionitumia nikiwa Tanzania na nilioenda kukutana nao Misri ni tofauti, kwa mfano mshahara tulikubaliana kwa mwezi Dola 2,000 (Sh5.2 milioni), ila nilivyoenda nikakuta wameniwekea Dola 1,000 (Sh2.6 milioni),” alisema Simba.

Aidha, mshambuliaji huyo alisema licha ya kukiukwa kwa makubaliano ya mshahara, lakini mkataba wa mwanzo walikubaliana pia atapangiwa nyumba ya kuishi na gari kwa ajili ya kutembelea, jambo ambalo uongozi wa klabu hiyo ulishindwa kulifanya.

Mshambuliaji huyo aliyezaliwa Julai 15, 2006, alijiunga na KMC katika dirisha dogo la Januari 2025 akitokea JKU ya Zanzibar na kuonyesha kiwango kizuri, baada ya kupata nafasi ya kuchezea timu za taifa za vijana chini ya miaka 20.

Endapo uhamisho huo ungekamilika, mshambuliaji huyo angekuwa ni mchezaji wa pili kwa misimu ya karibuni kutokea KMC kusajiliwa Misri, baada ya Rahim Shomaryaliyejiunga na Ghazl El Mahalla.

Rahim alijiunga na Ghazl El Mahalla Julai 14, 2025 ingawa baadaye alishindwa kufanya vizuri na kujiunga Singida Black Stars, Januari 26, 2026.