Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaze amuibua straika Kagera Sugar

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Polisi Tanzania, alisema ujio wa Kaze huenda ukabadilisha hali ya mwenendo wa kikosi hicho, japo wanapaswa kuendelea kupambana zaidi, ili kuendana na ushindani uliopo msimu wa 2026-2027. 

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Naku James Kazimoto amesema ujio wa kocha mkuu, Mrundi Cedric Kaze ni moja ya sehemu muhimu kwa wachezaji wa kikosi hicho kubadilisha upepo mbaya ambao umeikumba tangu kuanza kwa msimu huu.

Nyota huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea Polisi Tanzania, alisema ujio wa Kaze huenda ukabadilisha hali ya mwenendo wa kikosi hicho, japo wanapaswa kuendelea kupambana zaidi, ili kuendana na ushindani uliopo msimu wa 2026-2027.

“Tumekuwa na mwenendo usioridhisha ila kwangu naamini ni upepo mbaya tunaokutana nao, ujio wa kocha mpya ni sehemu pia nyingine ya mwanzo wa kila mchezaji kuonyesha zaidi ya uwezo wake ili kwa pamoja tuitoe timu hapa ilipo,” alisema Naku.

Aidha, mshambuliaji huyo aliyetamba na timu mbalimbali za Mbuni FC ya Arusha na Copco FC ya jijini Mwanza, alisema wao kama wachezaji wanaumia na mwenendo wanaopitia, japo ni mapema kukata tamaa kwa sababu wana uwezo wa kurekebisha mambo.

Kaze aliyetamba na timu mbalimbali za Yanga, Namungo FC za Tanzania, Mukura Victory Sports ya Rwanda na Atletico Olympic FC ya kwao Burundi, amejiunga na Kagera Sugar akichukua nafasi ya Juma Kaseja aliyeondolewa Septemba 21, 2026.

Mrundi huyo aliyefundisha Kaizer Chiefs FC na Sekhukhune United FC zote za Afrika ya Kusini na timu za taifa za vijana za Burundi chini ya miaka 17, 20 na 23, huku akihudumu kocha msaidizi kwa wakubwa, amebeba matumaini ya Kagera Sugar.

Kaseja aliyewahi kuitumikia Kagera Sugar akiwa mchezaji na kocha wa makipa, huku akichezea pia Simba, Yanga na timu ya taifa ya Taifa Stars, alikiongoza kikosi hicho kurejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka 2024-2025.

Kwa msimu wa 2026-2027, Kaseja aliiongoza Kagera Sugar katika mechi sita za Ligi Kuu bila ya ushindi baada ya kutoa sare mbili na kupoteza nne.