Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Del Piero aweka mikakati Bigman FC

DEL PIERO Pict

Muktasari:

  • Del Piero ni kocha wa tatu kuifundisha Bigman FC msimu huu, baada ya watangulizi wake Amanzi Nurdin na Omary Kapilima, ambapo timu hiyo imecheza mechi tisa, ikishinda mitatu, sare moja na kupoteza mitano, ikiwa nafasi ya 10 na pointi 10.

KOCHA Mkuu wa Bigman FC, John William Zongwe 'Del Piero' amesema bado ana kazi kubwa ya kutengeneza kikosi bora na cha ushindani msimu huu, japo mwenendo wa kiuchezaji wa wachezaji wa timu hiyo unampa matumaini ya kufanikisha malengo hayo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Del Piero amesema hadi kufikia raundi 15, za kwanza ndipo atakapoona mwelekeo mzima wa timu hiyo msimu huu, licha ya kukiri ushindani umekuwa mkubwa zaidi hasa kutokana na mahitaji na malengo ya kila mmoja wao.

"Kwa sasa ni vigumu kusema nitaipambania timu ipande daraja kutokana na kipindi kigumu nilichokikuta, ila ninachoweza kusema nitahakikisha naipigania inabakia Championship kwa msimu ujao kwa lengo la kujipanga vizuri," amesema Del Piero.

Kocha huyo aliyezifundisha Namungo FC, Pan African FC, TMA FC, Mafunzo SC ya visiwani Zanzibar, amejiunga na Bigman FC huku mara ya mwisho aliifundisha IAA SC ya Arusha, ikiwa Ligi Daraja la Pili, ingawa kwa sasa inashiriki Championship.

Del Piero ni kocha wa tatu kuifundisha Bigman FC msimu huu, baada ya watangulizi wake Amanzi Nurdin na Omary Kapilima, ambapo timu hiyo imecheza mechi tisa, ikishinda mitatu, sare moja na kupoteza mitano, ikiwa nafasi ya 10 na pointi 10.