Kabadi Zanzibar mechi nne bila ushindi
Muktasari:
- Timu hiyo imeendelea kupata matokeo mabaya katika mashindano hayo yanayoendelea kuchezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.
WAKATI Zanzibar ikiwa mwenyeji wa michuano ya mchezo wa Kabaddi Afrika, imepokea kichapo katika michezo minne mfululizo.
Timu hiyo imeendelea kupata matokeo mabaya katika mashindano hayo yanayoendelea kuchezwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.
Katika mchezo wa kwanza, Zanzibar ilifungwa na Uganda kwa pointi 45-25, ilipoteza tena dhidi ya Malawi kwa kufungwa pointi 38-36 katika pambano lililokuwa na ushindani mkubwa.
Timu hiyo imeendelea kuteseka katika mchezo wa tatu baada ya kipigo cha pointi 55-18 dhidi ya Kenya ambayo ilitawala kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Mchezo wa nne, Tanzania iliibuka na ushindi wa pointi 42-37 dhidi ya Zanzibar.
Kwa upande mwingine, timu ya Kenya imeonekana kuwa na upinzani mkubwa baada ya kuifunga Tanzania pointi 51-18, mchezo uliokuwa na ushindani mwanzo hadi mwisho.