Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Juma Shaaban aziweka tatu mezani

SHAABAN Pict

Muktasari:

  • Uongozi wa klabu hiyo unaona kumsajili beki huyo kutasaidia kuongeza ushindani na kuimarisha uwezo wa timu.

WAKATI mchezaji Juma Shaaban ‘James’ akiachana na KVZ, JKU, Uhamiaji na Black Sailors zinatajwa kuingia kwenye mbio za kuwania saini ya beki huyo.

Taarifa kutoka vyanzo vya karibu na klabu hizo, zinaeleza viongozi wa JKU wanaamini James anaweza kuongeza nguvu katika safu yao ya ulinzi kuelekea msimu ujao.

Uongozi wa klabu hiyo unaona kumsajili beki huyo kutasaidia kuongeza ushindani na kuimarisha uwezo wa timu.

Pia, Black Sailors imeonekana kuwa miongoni mwa timu zinazomfuatilia kwa karibu mchezaji huyo, ikiamini uzoefu na uwezo wake unaweza kuwa silaha muhimu katika harakati za kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti, mchezaji huyo amesema bado timu hizo hazijamtafuta hadi sasa ingawaje inasemekana zinamuhitaji.

“Ni kweli hizo timu zinahitaji lakini hatujakaa chini kuzungumza kuhusu hilo lakini wasisite kwani mimi nipo huru kwasasa,” amesema.

Amesema, kwasasa ameshaachana na KVZ na bado hajafanya mazungumzo na timu yoyote, hivyo inayomhitaji inakaribishwa mezani kukubaliana.